LIVE STREAM ADS

Header Ads

ZOEZI LA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA MWANZA LAKWAMBA.

Zoezi la Uandikishaji na Uboreshaji wa daftari la kudumu la Wapiga Kura Mkoani Mwanza limeshindwa kuanza hii leo, licha ya kuelezwa kwamba vifaa zaidi ya Mia tano kwa ajili ya zoezi hilo vimekwisha kuwasili Mkoani hapa.

Duru za habari zinaeleza kuwa uandikishaji huo umeshindwa kuanza Mkoani hapa, ili kupisha semna elekezi iliyoanza jana kwa wasimamizi wa zoezi hilo ambalo la uandikishaji ambalo linaendeshwa kwa kutumia mfumo wa Kisasa wa Kielektroniki Biometric Voter Registration (BVR).

Kutokana na mabadiliko hayo ya Uandikishaji na Uboreshaji wa daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Mwanza, zoezi hilo linatarajiwa kuanza June Tisa Mwaka huu ambapo wananchi wote wenye sifa ya kujiandikisha wanahimizwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kushiriki katika zoezi hilo.

Kwa mjibu wa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC, zoezi la uandikishaji wa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura lilitarajiwa kuanza leo June Mbili katika Mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga na Simiyu na kufikia tamati Julai Nne mwaka huu.

No comments:

Powered by Blogger.