LIVE STREAM ADS

Header Ads

WIKI YA MAZINGIRA YAZINDULIWA MKOANI MWANZA. JAMII YAHIMIZWA KUYATUNZA.

Picha ya Pamoja katika uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Mkoani Mwanza baada ya zoezi la kupanda miti lililofanyika katika Shule ya Sekondari Buhongwa.
 Na:George GB Pazzo
Jamii imetakiwa kuwajibika katika Upandaji wa Miti pamoja na utunzaji wa Mazingira kwa ujumla, kwa lengo la kupamban na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchini.

Afisa Mazingira Jiji la Mwanza Charles Amani ametoa kauli hiyo hii leo, wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Mazingira duniani ulioambatana na zoezi la Upandaji wa Miti katika Shule ya Msingi na Sekondari Buhongwa.

Amani amesema kuwa upandaji wa Miti husaidia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo ni pamoja na ongezeko la joto duniani ambalo hutokana na shughuli za uzalishaji ikiwemo Viwanda.

Nae Naibu Meya wa Jiji la Mwanza John Austine Minja amefafanua kuwa miongoni mwa faida za upandaji wa Miti ni pamoja na kusaidia katika uzalishaji wa hewa aina ya Oxygen ambayo husaidia katika upumuaji wa mwanadamu hivyo ni vyema wananchi wakawa na desturi ya kupandaji miti na kutunzaji mazingira.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Buhongwa wameiomba Serikali kufikisha elimu ya Upandaji na Utunzaji wa Miti katika jamii mara kwa mara ili kuwawezesha wanajamii kutambua umhimu wake.


Shughuli mbalimbali za utunzaji wa Mazingira zinatarajiwa kufanyika katika Maadhimisho hayo ya wiki ya Mazingira Duniani ambayo yameanza kuadhimishwa hii leo Juni Mosi hadi June Tano Mwaka huu ambapo Kilele cha Maadhimisho hayo Kimkoa kinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Gandh Hall huku Kitaifa kikifanyika Mkoani Tanga.
Picha ya Pamoja Buhongwa Sekondari
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Buhongwa Jijini Mwanza
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Buhongwa Jijini Mwanza
Naibu Meya wa Jiji la Mwanza John Augustine Minja akipanda Mche
Mrashy Diana Manyilizo ambae ni Mwenyekiti wa Asasi ya Uchungu na Mwana Mkoani Mwanza akipanda Mche
Miti ni Uhai
Zoezi la Upandaji wa Miche katika Shule ya Sekondari Buhongwa
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Buhongwa Jijini Mwanza
Charles Amani ambae ni Afisa Mazingira Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Mwenye Kinasa sauti) akizungumza katika uzinduzi wa Wiki ya Mazingira
Wiki ya Mazingira Duniani katika Mkoa wa Mwanza imeandaliwa kwa ushirikiano wa karibu na Ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Taasisi na Asasi binafsi Mkoani Mwanza (Mwanza Non-Government Organization Network-MNGON, Kampuni ya Utengenezaji wa Mabati ya ALAF ambayo ni Rafiki wa utunzaji wa Mazingira pamoja na Jiji la Tampere la nchini Finland.
John Minja (Mwenye Miwani) ambae ni Naibu Meya wa Jiji la Mwanza akizungumza
John Minja akisalimiana na Wanafunzi wa Buhongwa Sekondari
Mrashy Diana Manyilizo ambae ni Mwenyekiti wa Asasi ya Uchungu na Mwana Mkoani Mwanza akizungumza kwa niaba ya Asasi nyingine.
SOMA BANGO KWA UMAKINI.

No comments:

Powered by Blogger.