HII NDIYO KAULI YA CCM MKOANI MWANZA KUHUSIANA NA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Mwenye Miwani akiwasili katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza juzi jumamosi.
Na:George GB Pazzo
Wananchi
Mkoani Mwanza wameshauriwa kujitokeza kwa Wingi kwa ajili ya Kujiandisha katika
daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kupata sifa ya kushiriki katika zoezi la
Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi August Mwaka huu.
Ushauri huo umetolewa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa
Mwanza Miraji Mtaturu, wakati akiwahutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara
uliofanyika juzi katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza.
Mtaturu ametoa rai kwa kila mwananchi aliefikisha Umri wa Miaka 18 na
kuendelea kuhakikisha kuwa anajiandikisha katika daftari la kudumu la Wapiga
Kura, lengo likiwa ni kutumia haki yake ya Kikatiba ya kuwachagua viongozi
atakaoshirikiana nao katika shughuli za kimaendeleo.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda amewasihi
wanasiasa kuacha kuwagombanisha wananchi kutokana na itikadi za Kivyama katika
kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu ambapo amewasihi wanasiasa wenye
tabia hiyo kuwa na siasa za kiustarabu wawapo Majukwaani.
Nae John Lipes Kayombo ambae ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
(MNEC) anaewakilisha Vyuo Vikuu nchini, amewasihi wanafunzi wote wa Vyuo Vikuu
nchini kuwa watulivu na kuachana na Migomo isiyo na tija katika kipindi hiki
cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu ambapo amebainisha kuwa tayari kuna mipango
madhubuti ya kuhakikisha kuwa wanafunzi ambao hawajapata mikopo yao wanapata
mikopo hiyo kwa wakati.
Kwa mjibu wa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini, zoezi la
uandikishaji wa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura linatarajiwa
kuanza kesho June Mbili katika Mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga na Simiyu
ambapo litafikia tamati Julai Nne mwaka huu.
John Lipes Kayombo ambae ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) anaewakilisha Vyuo Vikuu nchini
Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda (Kushoto) akifuatiwa na Hussein Kim ambae ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Nyamagana (Katikati) pamoja Henry James ambae pia ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ilemela.
Wananzengo!
No comments: