MAKALA: "UMUHIMU WA KUFUATA NDOTO YAKO" SEHEMU YA TATU.
Bonyeza HAPA Kusoma Sehemu ya Kwanza na ya Pili then Twnde sawa.
Maisha hayana maana kama hauna kitu cha kutoa/kuwapa wenzako katika dunia hii, mtu anapoamua kufuatilia ndoto yake mpaka ikatimia inamaanisha anakuwa ameipa/ametoa kitu fulani kwa jamii yake ambacho kinakuwa na thamani, usikubali kuishi tu pasipo kutoa mchango fulani katika jamii yako. Kuwa na mtazamo wa kuona kwamba unatakiwa kuchangia katika jamii yako siku zote, hii itakufanya ujione ni mtu mwenye majukumu na unatakiwa kufanya mambo fulani ili kuleta mabadiliko na mchango katika jamii yako.
Jack Ma(alibaba) alipoenda Marekani mwaka 1995 na kukuta maendeleo ya internet (mtandao)kule alishangaa sana, alijaribu kuangalia kama kuna kitu chochote kutoka china kipo kwenye mtandao lakini hakupata kuona hata kimoja, aliamua kuanzisha biashara ya kuuza vitu kwenye mtandao kwa kutumia jina la Alibaba, hii ilisaidia watu wa China kuweza kununua vitu Marekani na wa marekani kununua vitu kutoka China na biashara yake hii imekuwa na ninavyoandika hapa Alibaba ana utajiri wa zaidi ya $25.3bill na ni tajiri wa 33 duniani huku akiwa tajiri wa kwanza China, alichofanya hapa alichangia kwenye jamii yake kwa kuwawezesha kupata vitu toka sehemu mbalimbali za dunia. Kwa hiyo ndoto yako itakusaidia kuchangia jambo fulani katika jamii yako.
Wewe kuamua kufuatilia ndoto yako unatoa tumaini na msukumo kwa wengine ambao wanataka kuanza kufanyia kazi ndoto zao,lakini pia kwa kuwapa tumaini watu wengine katika kufanya na kutimiza ndoto zao na sisi pia tumaini letu linakuwa kubwa zaidi, maana kitu unachokituma kwa wenzako kinakurudia tena wewe, Mwalimu wangu Jihn Rohn aliwahi kusema "As we inspire others we get inspired"(yaani tunapowapa watu msukumo fulani katika kutenda jambo lao na sisi tunapata ule msukumo) ila kama ukiamua kutokufanya inamaanisha hawatakuwa na tumaini kwamba siku moja nao watatimiza ndoto zao, kwani mara ngapi umekuwa ukisikia watu wanasema duuu mimi ninampenda yule kaka au yule dada maana hakati tamaa katika kile anachokitenda kila siku anapambana na anakuja kwa namna mpya na nzuri ya kuvutia.
Lakini pia kadiri unapokuwa unafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha unatimiza ndoto yako ndio kiasi cha kutokushindwa kwako katika ndoto yako kinapungua, utajikuta kwamba unafanya vitu vikubwa na vya ajabu ,utagundua mambo mengine makubwa na ya ajabu ambayo unayo lakini hukuwahi kuyafahamu kwa sababu tu hukuamua kufanyia kazi ndoto yako, lakini pia utajikuta kwamba unakutana na watu wengi wengine ambao hukuwahi hata kufikiri ungekutana nao, Na hiki ndio kile kipindi ambacho mtu huwa anajifunza kwamba hakuna kitu ambacho mtu anashindwa kukitimiza katika maisha yake ali mradi tu awe kaamua kutoka ndani kwenye kilindi cha moyo wake.
Ndoto pia zina nguvu ya kutosha kuelezea mimi au wewe ni watu wa aina gani na tunaweza tukafanya nini katika maisha yetu ambayo tunaishi, vuta picha ni kipi kitatokea wakati umeshatimiza ndoto yako, je jamii yako itakuchukuliaje, utajisikiaje, na utakuwa umechangia kiasi gani katika jamii yako ambayo unaishi. Kubwa zaidi itakuonesha wewe ni mtu wa namna gani na unaweza kufanya nini katika jamii yako.
IMEANDALIWA NA LIFE SECRETS COMPANY YA JIJINI MWANZA AMBAO NI WATAALAMU WA AFYA NA MAENDELEO BINAFSI.
Email:allnhumph@gmail.com Phone: 0689 45 26 70/0765 53 68 42
No comments: