LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA WILAYA YA NYANG’WALE MKOANI GEITA ATISHIA KUWAHAMISHA WANAKIJIJI WA NG'WASABUKA.

Dc Nyang'wale Mkoani Geita Ibrahim Marwa akizungumza katika shughuli ya Ufunguaji wa Moja ya Migodi katika Wilaya yake hivi karibuni.
Na:Shabani Njia
Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale  Mkoani Geita Ibrahimu Marwa ametishia kuwahamisha wakazi wa kijiji cha Ng’wasabuka kata ya Mwigilo kwa kile kinachodaiwa kuwepo kwa machimbo mapya ya Madini ya Dhahabu yaliyoibuliwa na wachimbaji wadodo wadogo.

Hayo yalibainishwa juzi na wachimbaji wadogo wadogo wa Kijiji hicho ambapo walibainisha kuwa kila wanapoibua machimbo mapya huvamiwa na Serikali  kwa madai kuwa maeneo hayo ni mali ya wawekezaji wakubwa jambo ambalo sio sahihi.

Mmoja wa wachimbaji hao Charles Kapongo alisema kuwa wamekuwa wakipokea vitisho kutoka kwa Jeshi la Polisi wilayani humo kwa misingi ya kutumiwa na mkuu huyo wa Wilaya ambae wanasema aliwaambia kuwa eneo la kijiji hicho ni mali ya mwekezaji wa kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi wa Bulyanhulu.

Kwaupande wake afisa madini Mkoa wa Geita Musimu Kabasa alisema kuwa walifanya mkutano wa pamoja na wachimbaji hao sambamba na mwekezaji na uongozi wa ofisi ya mkuu wa Wilaya hiyo na kukubaliana na wachimbaji hao kutoka eneo katika hilo ndani ya mwezi mmoja lakini imekuwa tofauti baada ya wananchi wa kijiji hicho kukimbilia tena kwa viongoziwa siasa na kueleza kutokuwa tayari kuondoka kijijini hapo.

Akijibu malalamiko hayo, mkuu huyo wa Wilaya ya Nyang’wale Ibrahimu Marwa alisema kuwa wachimbaji hao wamekuwa wakiendesha shughuli za uchimbaji katika eneo la kijiji hicho kinyume cha sheria za Madini na kuongea kuwa eneo wanalochimba lina leseni ya mwekezaji wa kampuni ya Acacia hivyo kama watakaidi kuondoka kwa hiari, wataondolewa kwa nguvu.

No comments:

Powered by Blogger.