LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKALA: KIJANA HII INAKUHUSU HIVYO USIPUUZIE.

Imeandaliwa na Life Secrets Company
Unajua ukikaa chini ukitathimini kipindi cha ujana ni kifupi sana katika maisha yako. Kitabu kilichoandikwa miaka 3500 iliyopita kinasema kwamba mtu hujifunza uvumilivu kipindi cha ujana, hakuna uvumilivu kwenye uzee, pindi mtu atakaposhindwa kuutumia ujana wake vizuri atateseka sana kwenye uzee wake.

Leo hii wazee wote unaowaona wanaangaika kufanya kazi ngumu mjini huku wana miaka 60 na kuendelea wengine hata ofisi walizo hawataki kustaafu vijana wapate kazi ni dhahiri kwamba hawakuutumia vizuri ujana wao,hawakupangilia namna ambavyo watakavyoishi pindi watakavyozeeka. Na wewe kijana unaesoma hapa usipojipanga vizuri nawe katika uzee wako utakuwa hivyo hivyo.

Jipigie mahesabu yakinifu utagundua kwamba ukimaliza form 6 utakuwa na miaka 18 , weka chuo miaka 5 weka miaka 2 ya kutafuta kazi au kujiajiri inafika miaka 25 kama ulichelewa shule au ulirudia miaka itaongezeka zaidi ya 25 haya unatakiwa kujenga na pia unatakiwa kuoa utengeneze familia pindi ufikapo miaka 30.

Ujana unakuwa kati ya miaka 18-35 ina maana kama hukujipanga vizuri utashangaa na ujana unapita hujaoa, huna nyumba, na hujajiweka safi kimaisha kama ukiwa mzembe zaidi utajikuta hata nyumbani kwenu haujatoka na hapa ndipo kujikataa na kuona ni ngumu kufanikiwa huwa kunaanzia kama uwo umri wa miaka 35 utakukuta kwenu.

Kimsingi vijana wanazo faida mbili kubwa ambazo ni kwamba wanaweza kutumia akili zao na pia wanazo nguvu katika kutenda jambo fulani, watu wazima wao hawana nguvu sana huwa kwa kiasi kikubwa wana akili tuu na nguvu kidogo na ndio maana watu ambao wanajua siri hii huwa kuna umri wakifika wanawekeza kwa vijana wenye vipaji mwangalie Meneja Said Fela anachofanya ndio utanielewa.

Ujana ni kipindi ambacho unatakiwa kuwa na nidhamu ya ya hali ya juu. Nidhamu tulikuambia ni uwezo wa kuweza kutawala akili na mwili wako. Ukiwa na nidhamu kipindi cha ujana wako itakusaidia katika mambo mengi muhimu.

Na nidhamu hii inaanzia kwenye kuheshimu watu, kujiheshimu mwenyewe haswa mwili wako,kujua namna ambavyo unatakiwa kuongea na watu wa rika lako na watu wazima.

Lakini pia nidhamu ipo mpaka katika kuvaa ,muonekano, na kile ambacho unakiingiza katika akili yako, sio kila kitu ni cha kuingiza akilini mwako kuna vitu vingine ni lazima ujifunze kuvikwepa ikiwemo kukwepa watu ambao wanaokuletea mawazo ya kushindwa,watu wenye mitazamo hasi, watu wanaolalamikia serikali kila siku,watu wasiotaka kufikiri na kujituma.

Ukiwa kama kijana pia ni lazima kujifunza umuhimu wa kumezea mambo haswa yale ambayo unayasikia na huna uhakika nayo naomba niseme ivi sio kila neno unalolisikia una haki ya kulisema mengine unamezea. Kuna mtu aliwahi kusema No research no right to talk, yaani kama huna utafiti hauna haki ya kuongea kuwa makini sana katika hili wengi wameanguka kwa maneno yao wenyewe.

Ukiwa kama kijana ni lazima ujue maneno hayana tofauti na mbegu neno unalolitamka linaweza likajenga au likabomoa urafiki wako na mtu fulani. Kama huamini nenda kamseme rafiki yako vibaya alafu ajue uone nini kitatokea.

Tunajua fika kabisa ni vigumu kuzuia rafiki yako au ndugu yako kukudharau lakini kuna namna ambayo unaweza ukaishi akakuheshimu. Ukijiweka kirahisi rahisi, hujiheshimu, ni dhahiri utadharaulika. Lakini ukijiheshimu, ukifanya kazi kwa bidii, ukijifunza namna ya kuongea na watu ni dhahiri utaheshimika.

Hebu jifunze katika hiki kidogo,muombe Mungu akusaidie,fanya kazi kwa bidii, kuwa na marafiki sahihi, jifunze katika makosa, jifunze kutumia muda wako vizuri na usimruhusu mtu awaye yeyote akaudharau ujana wako.
Tutumie Makala au tukio lolote; 
binagimediagroup@gmail.com/ 0757 43 26 94

No comments:

Powered by Blogger.