LIVE STREAM ADS

Header Ads

MTUHUMIWA SUGU WA GENGE LA MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI NCHINI ATIWA MBARONI.

(Picha Haihusiani na Habari hii)
Na:Shaban Njia & Vesterjtz
Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga, linamshikilia mtuhumiwa mmoja anayesadikika kujihusisha na mauaji ya walemavu wa Ngozi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Akizungumuza jana na wandishi wa habari kwa niaba ya kamandawa polisi Mkoani shinyanga Justus Kamugisha, Kamanda wa polisi wilayani Kahama Leonard Nyandahu alimtaja mtuhumiwa huo kwa jina la Mwanakulya Kapani miaka (45).

Nyandahu alisema kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akisakwa na jeshi la Polisi ambapo limefanikiwa kumnasa juzi katika kijiji cha Shilela kata ya Lunguya wilayani humo majira ya saa nane usiku nyumbani kwa wazazi wake.

Mtuhumiwa huyo ni miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa kufuatia tukio la kumuua mlemavu wa Ngozi Esta Charles katika kijiji cha shilela mwezi August 29,2008 ambao ni Masumbuko Madata, Charles Kalamji na Medad Maziku waliokwisha hukumiwa kunyongwa.

Hata hivyo jeshi hilo linaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo ikiwa ni pamoja na kubaini mtandao wa watu wanaojihusisha na mauaji ya  walemavu wa ngozi nchini ambapo uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu shitakata linalomkabili.

No comments:

Powered by Blogger.