LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANACHAMA WA YANGA TAWI LA MWALONI KIRUMBA JIJINI MWANZA WAIBUKA NA HII MIPANGO JUU YA TIMU YAO.

Na:Oscar Mihayo
Wanachama wa Young African SC (Yanga) Tawi la Mwaloni Kirumba Jijini Mwanza, wanatarajia kufanya sherehe ya kipekee juu ya ubingwa wa 25 wa timu hiyo ikiwa ni pamoja na kuadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.

Akiongea jana ofisini kwake katibu wa tawi hilo Emmanuel Majura alisema kuwa sherehe hiyo inatajiwa kuwa ya kipee na itafanyika mwanzoni mwa nwezi ujao mara baada ya kumalizika kwa mfungo mtukufu wa ramadhani.

Majura aliongeza kuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo anatarajiwa kuwa mwenyekiti wa matawi yote ya Yanga kutoka Jijini Dar es salaam Mohamed Msumi ambapo mara baada ya sherehe hiyo itapigwa mechi ya mashabiki wa simba na Yanga katika uwanja wa magomeni kirumba.

Alisema lengo kubwa la kufanya sherehe hiyo ni kukutanisha wanachama, kufahamiana na kuongeza wanachama wapya kwa kuwapatia kadi na kupanga amshaamsha ya timu hiyo pindi itakapo kuwa inacheza mara baada ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Sisi tangu tuanzishe tawi letu hapa mwaloni hatukuwai kufanya sherehe yoyote na kukutana kwa pamoja hivyo tumeona hii ni nafasi pekee ya kukutana na kujadili mambo ya msingi ndani ya timu yetu huku tuadhimisha miaka 80 ya timu ya kuanzishwa kwake.” Alisema Majura.

Aidha Majura alitoa rai kwa uongozi tawi ngazi ya Mkoa chini ya mwenyekiti wake mzee Mnisi kufanya uchaguzi wa viongozi wapya kwa kuwa uongozi wao umeongoza kwa muda mrefu bila kufanyiwa mabadiliko.

Pamoja na hayo pia aliwataka wapenzi wote na wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi ikiwa pamoja na kuwasilisha michango yao kwa waratibu wao ili waweze kupanga bajeti mapema.

No comments:

Powered by Blogger.