LIVE STREAM ADS

Header Ads

SIKILIZA WALICHOKISEMA KATIKA USAILI WASHIRIKI WA BONGO STAR SEARCH 2015 MKOANI MWANZA.

Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmack Production inayoandaa shindano la Bongo Star Search Rita Paulsen a.k.a Madam Rita, katika Judge Master J na Kulia ni Jugde Salama Jabir wakiwa katika usaili Mkoani Mwanza ambapo Wasanii Sita wataiwakilisha Mwanza hivyo usikose kufuatilia Star Tv na Clods Tv kuanzia Julai 19, 2015.
Na:George GB Pazzo
Baadhi ya Washiriki waliojitokeza Wikendi iliyopita katika Usaili wa Kusaka nafasi ya Kushiriki katika Shindano la Kutafuta waimbaji la Bongo Star Search 2015 Mkoani Mwanza, wamedokeza kuwa zoezi la usaili lilikuwa gumu kutokana na wasanii waliojitokeza kila mmoja kujiandaa vya kutosha.

“Mchakato ulikuwa mgumu kiasi fulani maana vipaji vilikuwa ni vingi na wasanii wanaimba vizuri na naweza kusema hata mimi kuna watu nimewaapriciate na ikitokea wao ndio wakashinda kwa safari ya kwenda Dar es salaam kwa BSS I will be very glad and happy for them...”. Alibainisha Msanii Shazimin Karim kutoka Kahama Mkoani Shinyanga.

“Aaaa mimi nimepata nafasi ya saba na walikuwa wakitafuta washiriki sita hivyo nimekosa nafasi na nimeyakubali matokeo maana asiekubali matokeo si mshindani lakini kutoka kwangu ni kuanza njia mpya yaani nitajipanga upya…”. Alisema Msanii Fadhiri Julius kutoka Pasiansi Ilemela Mkoani Mwanza.

Bonyeza HAPA Kutazama Picha za BSS 2015 Mwanza.

Bonyeza Play hapa chini Kusikiliza Mahojiano

No comments:

Powered by Blogger.