LIVE STREAM ADS

Header Ads

NAYAKUMBUKA HAYA WAKATI NAKUPONGEZA KATIKA SIKU YAKO YA KUZALIWA, GSENGO WA JEMBE FM NA GSENGO BLOG.

GB Pazzo (Kushoto) pamoja na Gsengo (Kulia)
Na:George GB Pazzo
Anaitwa Albert George Sengo (Gsengo). Kwa wadau wa tasnia ya Utangazaji na Habari nchini watakuwa wanamfahamu vizuri sana mwanaharakati huyu ambae amebobea katika Masuala ya Utangazaji, Habari pamoja na utengenezaji wa Matangazo. 

Sitaki niwachoshe sana lakini historia yake katika tasnia ya habari na utangazaji ilianza kitambo kidogo tangu akiwa Jijini Arusha akifanya kazi na Radio ya Watu Clouds Fm kabla ya kuhamia Jijini Mwanza ambapo pia alifanya kazi na radio hiyo kwa muda mrefu hadi pale alipojiunga Radio Mpya Jijini Mwanza iitwayo Jembe Fm mwishoni mwa mwaka jana.

Ni mmoja kati ya watu poa sana, anaejali na kusaidia kadri awezavyo. Nikimzungumzia Albert Gsengo nakumbuka namna mtandao huu (Binagi Media Group) ulivyoanza kipindi hicho ukiitwa Mtanzaniamedia Blog. Hakika alikuwa mmoja wa watu waliotia juhudi katika kuhakikisha kwamba mtandao huu unafikia malengo yake ambayo leo hii tunayaona japo bado safari ni ndefu.

Yote hayo nayaongea tu japo kwa leo si muhimu sana, kwani kwangu jambo la Muhimu katika siku hii ya leo ambayo ni Julai 24, 2015 ni kukumbuka SIKU YA KUZALIWA KWAKE ALBERT GEORGE SENGO (Gsengo) naliezaliwa tarehe na mwezi kama leo ikiwa ni miaka kadhaa iliyopita.

Hakika ninayo furaha kubwa kuandika ujumbe huu NIKIMTAKIA KILA LA KHERI MPAMBANAJI HUYU (GSENGO) katika siku yake hii ya kuzaliwa lakini pia katika maisha yake na Mola azidi kuibariki kazi ya Mikono na Sauti yake maana kubarikiwa kwake ni kubarikiwa kwetu sote na jamii nzima kwa ujumla.

Yapo mengi sana ya kusema ila kwa sasa naishia hapa, na nirudie tena kusema HAPPY BORN DAY MPAMBANAJI ALBERT GEORGE SENGO (GSENGO).
Powered by Blogger.