LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAIGIZAJI 15 JIJINI MWANZA WAPATA SHAVU KATIKA KAMPUNI YA SHAFINEYZ FILM PRODUCTION.

Picha ya Pamoja
Na:George GB Pazzo
Jumla ya waigizaji wachanga 15 Jijini Mwanza wamefanikiwa kuchaguliwa kujiunga na Kampuni Mpya ya Utengenezaji wa Filamu hapa nchini iitwayo SHAFINEYZ FILM PRODUCTION ya Jijini Mwanza, baada ya kupenya katika Usaili wa Kusaka Vipaji vya Uigizaji uliofanyika jana katika Ukumbi wa Lunala Hotel iliyopo Buzuruga Jijini Mwanza.

Akizungumza jana mara baada ya Usaili huo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Shafineyz Film Production, Shafineyz Abdallah alisema kuwa Kampuni yake imenuwia kuubadilisha Ulimwengu wa sanaa ya Uigizaji hapa nchini hususani katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ukiwemo Mkoa wa Mwanza kutokana na hivi sasa bado tasnia ya uigizaji kuwa duni katika Mikoa hiyo.

Alisema mbali na kuhakikisha kwamba anainua soko la Uigizaji Jijini Mwanza na Mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, pia Kampuni yake ya Shafineyz inatarajia kuleta mapinduzi kwa waigizaji kwa kuwaboreshea maslahi yao ambapo alibainisha kuwa waigizaji waliochaguliwa katika usaili uliofanyika jana wakionyesha Uwezo mzuri wa Kuigiza moja kwa moja watakuwa amenufaika na mkataba mnono ambao umeandaliwa na Kampuni yake.

Mfaume Makoba a.k.a FBI ambae alikuwa Chief Judge pamoja na Yusuph Kapama ambae alikuwa Jugde namba moja katika usaili huo kwa pamoja walibainisha kuwa Jiji la Mwanza lina vipaji vingi na vizuri vya Uigizaji, lakini vipaji hivyo havijaweza kuendelezwa jambo ambalo limeua soko la uigizaji Jijini Mwanza.

Walisema wanaamini kuwa wale waliochaguliwa kujiunga na Kampuni ya Shafineyz Film Production wamepata mwanya wa vipaji vyao kuonekana ambapo waliwataka waliopata fursa hiyo wazidishe juhudi zaidi ili nafasi waliyoipata iweze kuwaletea matunda chanya katika uigizaji huku wakiwasihi wale waliokosa nafasi kuzidisha juhudi zaidi ili wakati mwingine nao wapate fursa kama wenzao waliyoipata.

Nae Yuskiss Kisiba ambae ni Mhariri Mkuu wa Video katika Kampuni hiyo ya Shafineyz Film Production alisema kuwa Kampuni hiyo inatarajia kuingiza sokoni Filamu mpya za aina mbalimbali ambazo alisema kuwa anaamini zitaleta mapinduzi ya Uigizaji Jijini Mwanza pamoja na Tanzania nzima kwa ujumla ambapo aliwaasa wapenzi wa Filamu za hapa nyumbani Tanzania kutegemea kazi nzuri kutoka mikononi mwake.

Baadhi ya Waigizaji waliofanikiwa kuchaguliwa katika Usaili wa Kujiunga na Kampuni hiyo ya Shafineyz Film Production walielezea furaha yao kutokana na kuamini kuwa Kampuni hiyo itaweza kuwaweka katika Ulimwengu mzuri wa soko la Uigizaji hapa nchini, nafasi ambayo walisema kuwa waliikosa hapo awali.

Kwa Upande wa wale waliokosa nafasi ya Kujiunga na Kampuni hiyo katika usaili walishindwa kuzuia hisia zao na kujikuta wakimwaga machozi huku wakisema kuwa wanajutia kuikosa fursa hiyo kwa kuwa waliitamani sana hususani ikizingatiwa kwamba wana vipaji vya uigizaji lakini wanakosa support ya kutosha Jijini Mwanza na ndiyo maana baadhi yao hukimbilia Jijini Dar es salaam ili kujaribu bahati yao.

Zaidi ya Waigizaji 80 kutoka Jijini Mwanza na Maeneo ya Jirani waliweza kujitokeza katika Usaili huo japo waliopata nafasi ya Kujiunga na Shafineyz Film Production ni waigizaji 15 tu ambao ni Pendo Gedion (Nyakato Mecco), Sarafina Simon (Nyakato Mecco), Violeth Kitomari (Igoma), Rachel Maganga (Nyakato National), Lister Charles (Nyakato Sokoni) na Suleiman Cassim Suleiman (Buzuruga).

Wengine ni Teddy Elias (Buzuruga), Victoria Alphonce (Buzuruga), Mariam Gaspel (Bugando), Aisha Mohamed (Bugando), Sajda Shehodha (Unguja Jijini Mwanza), Ramadhan Hamis (Nyakato Mecco), Abdul Rajab (Nyakato Mecco), Bahati Mtenga (Nyakato Mecco) pamoja na Frank Kasambaganya (Nyakato Mecco).
Picha ya Pamoja
Picha ya Pamoja
Picha ya Pamoja
Picha ya Pamoja.
Mapozi baada ya Usaili na hapa ndipo vipaji vinaanza kuonekana.
Katikati ni Video Editor wa Shafineyz Film Production Yuskiss Kisiba akiwa na baadhi ya waliofaulu katika Usaili.
Mkurugenzi wa Shafineyz Film Production Mr.Shafineyz Abdallah (Kulia) akiwa na Mmoja ya waliofaulu katika Usaili (Kushoto).
Kutoka Kushoto wa kwanza ni Mkurugenzi wa Shafineyz Film Production Mr.Shafineyz Abdallah, wa pili ni mmiliki wa Mtandao huu GB Pazzo, wa tatu ni mmoja wa waliofaulu katika usaili na wa nne ni Yusuph Kapama ambae alikuwa Judge katika Usaili.
Katikati ni GB Pazzo ambae ni mmiliki wa mtandao huu akiwa na baadhi ya waliofanikiwa kujiunga na Kampuni ya Shafineyz Film Production na aliechuchumaa ni Video Editor wa Kampuni hiyo Yuskiss Kisiba.

No comments:

Powered by Blogger.