LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIDEO YA JULIANA PATRICK-DEAR DIARY KUACHIWA SIKU YA BIRTH DAY YAKE NCHINI MAREKANI.

Msanii Juliana Patrick
Na:Jacob Malihoja
Juliana Patrick ambae ni binti wa Kitanzania anayeishi kwa ajili ya masomo Jijini Houston Texas nchini Marekani anatarajia kuachia video yake ya kwanza ya kibao chake kiitwacho "Dear Diary".

Video hiyo inatarajiwa kuachiwa siku ya birth day yake ambayo itakuwa ni July 12 mwaka huu jijini humo. 

Binti huyu ambaye anatimiza miaka 16 tarehe hiyo, mpaka sasa ameshaachia ngoma tatu ambazo zinafaya poa ile mbaya ambazo ni Dear Diary, Remember Me pamoja na We Are On A Roll. 

Hapa nchini ngoma hizo zinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio ikiwemo 99.4 Radio Metro Fm ya Jijini Mwanza pamoja na Radio Uhuru Dar es salaam. 

Kubwa zaidi Kibao cha Dear Diary kilipotoka tu mwishoni mwa mwaka jana kilipanda chati na kufikia Nambari mbili katika chati za muziki huko Texas nchini Marekani.

Hii ni Habari njema kwa Watanzania hususani Wasukuma kutoka Isolo Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza baada ya Mtoto wao, Binti yao, Mjukuu wao na hata mdogo wao Juliana Patrick nyota yake ya Muziki kung'ara vyema na hatimae kuipeperusha Vyema Bendera ya Tanzania katika Ardhi ya Marekani.

SIKILIZA NA KUDOWNLOAD DEAR DIARY HAPA

No comments:

Powered by Blogger.