LIVE STREAM ADS

Header Ads

TIMU YA SOKA YA BUSWELU VETRANI YAIGARAGAZA UKEREWE VETERANI NYUMBANI KWAO.

(picha haihusiani na habari).
Na:Osical Mihayo
Timu ya soka ya Buswelu Veterani ya Ilemela Mkoani Mwanza imeitandika timu ya Ukerewe Vetrani ya Wilayani Ukerewe nayo ya Mkoani Mwanza kwa mabao 2-1 katika mchezo wao wa kirafiki uliofanyika juzi katika uwanja Getruda Mongela uliopo Mjini Nansio Ukerewe.

Mabao ya timu ya Buswelu yaliwekwa kimiani na Martini Bantanuka kunako dakika ya 31 ya mpambano huo  kabla ya timu ya Ukerewe kusawazisha kupitia kwa Afande Joel na ubao kusomeka 1-1 lakini Busweru waliendelea kulisakama lango la timu pinzani na mnamo dakika ya 83 mfungaji wa bao la kwanza akaongeza bao la pili na la ushindi.

Mratibu wa mashindano hayo David Mpemba (maarufu kama Baba D) alisema kuwa mapokezi yalikuwa mazuri ikiwa ni pamoja na kukesha wanacheza ngoma ya dogoli jambo lililochagiza ushindi wao kwani walifanya mazoezi ya kutosha na kuahidi kudumisha mahusiano yao kwa kuwataka wenyeji wao nao wafike Jijini Mwanza ili kujioea mambo mazuri zaidi ya hayo.

Aliongeza kuwa kwa sasa timu yao iko vizuri na ina mpango wa kuendelea kujiimalisha kiafya kwa kucheza na timu ya Mwanza Starehe mwishoni mwa wiki hii katika uwanja wa nyumbani wa Buwelu sekondari.

Aidha, aliwataka wapenzi na wadau wa mpira wa soka kuwa nao bega kwa bega kwani mbali na kucheza wao bado wana timu changa ambayo wana ilea ya Buswelu United ambayo inashiriki ligi daraja la nne Wilayani Ilemela na kuwaomba kuwafadhili kwa mambo mbalimbali ili waweze kufanikisha malengo yao ya Soka kwa wana Buswelu.

Kwa upande wa Kiongozi wa timu ya Ukerewe, Moshi Kazimoto alishukuru kwa kumaliza vizuri mchezo huo huku akisema kuwa wasinge fungwa ila tu ni kwa sababu ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwani wachezaji wake wengi walikuwa na swaumu huku akihaidi kuifuata Buswelu Veterani Ilemela kwa lengo la kulipa kisasi cha kufungwa na timu hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.