LIVE STREAM ADS

Header Ads

CCM MAGU YAZINDUA KAMPENI ZAKE ZA UCHAGUZI MKUU KWA KISHINDO.

Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza kimezindua vyema Kampeni zake za Uchaguzi Mkuu, baada ya Umati Mkubwa wa Wananchi na Makada wake kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo.
Binagi Media Group
Pichani ni sehemu ya Umati huo ambayo imejitokeza katika Uwanja wa Mpira wa miguu uliopo Kata ya Magu Mjini ili kushuhudia uzinduzi huo ambao umeongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu.

Katika Mkutano huo, Mtaturu amewasihi wakazi wa Magu kuwachagua viongozi wanaotokana na CCM kuanzia Madiwani, Mbunge na Rais ili kwa pamoja washirikiane kwa ajili ya maendeleo yao ikiwa ni pamoja na kutatua kero ya maji ambayo imedumu kwa muda mrefu Wilayani humo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwahutubia wakazi wa Magu katika Mkutano wa Uninduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Magu Kiswaga Boniventura Destery (Kulia) katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho uliofanyika jana Wilayani humo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho Mgombea Ubunge Jimbo la Magu Kiswaga Boniventura Destery.
Mgombea Ubunge Jimbo la Magu Kiswaga Boniventura Destery akiwahutubia wakazi wa Magu ambapo amesema kuwa Matatizo yao anayajua hivyo wampe ridhaa ya kuwa mbunge wao kwa ajili ya utatuzi wa matatizo hayo ambayo ni pamoja na kero ya maji, Afya na Miundombinu.
kushoto ni Mke wa Mama Mgombea Ubunge Jimbo la Magu Kiswaga Boniventura Destery.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Mwenye kinasa sauti) akiwatambulisha wagombea Udiwani Jimbo la Magu
Wagombea Udiwani katika Kata za Jimbo la Magu wakitambulishwa
Wagombea Udiwani Viti Maalumu Jimbo la Magu wakitambulishwa kwa wananchi na wakazi wa Magu
Wagombea Udiwani Viti Maalumu Jimbo la Magu
Wengi pia walirudisha kasi za Vyama vingine vya upinzani ikiwemo Chadema na ACT Wazalendo na kupokea kazi za CCM
Wengi pia walirudisha kasi za Vyama vingine vya upinzani ikiwemo Chadema na ACT Wazalendo na kupokea kazi za CCM
Aliekuwa Katibu wa ACT Wazalendo Wilaya ya Magu (Mwenye Kinasa Sauti) akizungumza baada ya kupokea kadi ya CCM
Isack Zablon ambae ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Magu (Mwenye kinasa sauti) akizungumza jana katika Mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za chama hicho Wilayani Magu. Pembeni ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu.
Makada wa CCM pamoja na Wakazi wa Wilaya ya Magu wakifuatilia Sera katika Mkutano wa Uzinduzi rasmi wa Kampeni za CCM Wilayani humo
Makada wa CCM pamoja na Wakazi wa Wilaya ya Magu wakifuatilia Sera katika Mkutano wa Uzinduzi rasmi wa Kampeni za CCM Wilayani humo
Makada wa CCM pamoja na Wakazi wa Wilaya ya Magu wakifuatilia Sera katika Mkutano wa Uzinduzi rasmi wa Kampeni za CCM Wilayani humo
Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii

No comments:

Powered by Blogger.