LIVE STREAM ADS

Header Ads

UTPC YATANGAZA KUMBUKUMBU YA MAUAJI YA DAUDI MWANGOSI MWAKA HUU.

Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC) Abubakar Karsan akizungumza na Waandishi wa Habari jana Jijini Mwanza katika Ofisi za Umoja huo zilizopo Isamilo juu ya kumbukumbu ya Kifo cha Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi.
Na:George GB Pazzo
 "Akiwa mwandishi wa Habari wa Chanel Ten na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Iringa, Mwangosi aliuawa na polisi Septemba Mbili Mwaka 2012 akiwa kazini katika Kijiji cha Nyololo Mkoani humo wakati jeshi la polisi likijaribu kuzuia Mkutano wa kisiasa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema". Alisema Karsan.

Karsan alibainisha kuwa UTPC ilianza kumuenzi Mwangosi tangu mwaka 2013 kila ifikapo Septemba Mbili ambapo kumbukumbu hiyo huambatana na Mkutano Mkuu wa Umoja huo pamoja na kutoa tuzo ya Uandishi uliotukuka kwa mwandishi aliefanya kazi ambayo hata ingeweza kuhatarisha maisha yake. 

Alisema kwa mara ya Kwanza tuzo hiyo ambayo hutolewa kupitia mfuko wa Daud Mwangosi Media Support and Development Fund ilitolewa Jijini Mwanza Mwaka 2013 na ilichukuliwa na Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Absalom Kibanda.

"Wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa Habari wanatakiwa kuhudhuria kumbukumbu hiyo ambayo yanatarajiwa kufanyika Septemba 02, 2015 Jijini Dar es salaam ambapo Mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo Usalama wa Waandishi wa Habari katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu hapa nchini, Sheria ya Makosa ya Mtandaoni na ile ya urushaji wa Matangazo ya kieletroniki pamoja na kuangazia juu ya Mkutano Mkuu wa Intanet unaotarajia kufanyika Septemba 11 mwaka huu". Alidokeza Karsan.
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC) Abubakar Karsan
Wanahabari
Wanahabari

No comments:

Powered by Blogger.