LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHADEMA YAZINDUA KAMPENI ZAKE ZA UCHAGUZI MKUU. LOWASA AOMBA MAHABA KATIKA SANDUKU LA KURA.

Sehemu ya Umati wa Wananchi na Makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema pamoja na Washirika wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa ukiwa katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika katika Uwanja wa Jangwani Jijini Dar es salaam hii leo.
Na:Binagi Media Group
Chama cha Demokrasia na Maendeo Chadema kimezindua leo kimezindua harakati zake za Kampeni zake za Uchaguzi Mkuu Kitaifa, katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Jangwani Jijini Dar es salaam.

Chadema imezindua kampeni hizo chini ya mwamvuli wa Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa katika mkutano ambao umehudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi na makada wake pamoja na wale wanaotoka vyama washirika wakihudhuria kwa wingi.

Katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemkabidhi Ilani ya Uchaguzi Mgombea urais wa chama hicho ambae pia anaungwa mkono na Ukawa Edward Lowasa.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Ilani hiyo, Lowasa ametaja baadhi ya mambo yaliyomo ambayo yataboreshwa kuwa ni pamoja na maboresho katika sekta ya Elimu, Kilimo Afya, Ujenzi wa Reli ikiwa ni miongoni mwa masuala mengi ambayo amesema kuwa yako katika tovuti ya chama kwani kulingana na muda hawezi kuyaeleza yote.

Lowasa amehitimisha hotuba yake fupi kwa kuwaomba Watanzania kuonyesha mahaba waliyomuonyesha kwa kuhudhuria Mkutano huo katika sanduku la kupigia kura.

No comments:

Powered by Blogger.