MTATURU: PUMBAVU ZAO WANAOTAKA KWENDA IKULU KWA KUMWAGA DAMU.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwahutubia Wananchi na Makada wa chama hicho katika Mkutano wa hadhara wa Kuwanadi wagombea wake wa (Udiwani Kata ya Isamilo na Ubunge Jimbo la Nyamagana) uliofanyika jana katika Kata ya Isamilo Jijini Mwanza.
Na:Binagi Media Group
Katika Mkutano huo Mtaturu aliwahimiza Wananchi wa Kata ya Isamilo na Jiji la Mwanza kwa ujumla kuwachagua viongozi wanaotokana na CCM na siyo kurudia makosa kama waliyoyafanya mwaka 2010 kwa kuwachagua viongozi wanaotokana na upinzani na hivyo kudhorotesha shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Chama hicho Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula (Kulia) katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Kata ya Isamilo Jijini Mwanza.
Mgombea Ubunge wa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza Stanslaus Mabula akizungumza katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Kata ya Isamilo Jijini Mwanza.
Katika Mkutano huo Mabula aliomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana kwa kuwa anao uwezo wa kuitumikia nafasi hiyo ya uongozi akisema kuwa atahakikisha anasimamia vyema vipaumbele muhimu ambavyo ni uboreshaji wa Huduma za Afya, Elimu ya Msingi na Sekondari, Michezo, Miundombinu pamoja na utatuzi wa kero na malalamiko ya ardhi Jijini Mwanza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akimtambulisha Charles Marwa Nyamasiriri (Kulia) ambae ni mgombea Udiwani Kata ya Isamilo Jijini Mwanza kwa tiketi ya Chama hicho.
Mgombea Udiwani Kata ya Isamilo Jijini Mwanza kwa tiketi ya Chama cham Mapinduzi CCM Charles Marwa Nyamasiriri akizungumza jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata hiyo.
Nyamasiriri aliomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa diwani wa Kata ya Isamilo ili kuwatumikia katika maendeleo yao badala ya kuwachagua viongozi wanaokwenda kurumbana katika vikao vya halmashauri na siyo kushirikiana nao kwa ajili ya maendeleo yao.
Katika Mkutano huo Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu aliwakemea baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani wanaosema kuwa wako tayari kwenda Ikulu hata kwa kumwaga damu na kuhoji kuwa kama wao ni wakimbizi waondoke nchini na kuiacha nchi ikiwa na amani pamoja na mshikamano wake.
"Wengine wamesema wako tayari kwenda Ikulu hata kwa kumwaga damu. Pumbavu zao wakamwage damu za wake na watoto zao Watuachie Tanzania yetu. Kama wao ni wakimbizi waondoke sisi tutabaki na Tanzania iliyo moja yenye amani na mshikamano kwani nchi hii watu wakimwaga damu hata baraka za kwenda Madarakani hazitakuwepo tena". Alisema Mtaturu
No comments: