LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI YATAKIWA KUTOA ELIMU KWA WAZAZI NA WALEZI WENYE WATOTO WALIO NA ULEMAVU.

Mwalimu Frank Joseph akimfundisha  Mwanafunzi Enock Josia wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Huruma iliyopo Ilemela Mkoani Mwanza namna ya kuandika kwa kutumia mguu.
 Na:Judith Ferdinand
Serikali imetakiwa kutoa elimu kwa wazazi na walezi wenye watoto walemavu kutowaficha ndani ndani watoto hao kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki za msingi ikiwemo kupata elimu.

Wito huo alitolewa juzi na Mkurugenzi wa shule ya Huruma ambao ni ya watu walemavu Adrew Jacob iliyopo Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.

“Naiomba serikali itoe elimu kwa wazazi wenye watoto walemavu waache kuwaficha nyumbani kwani wanapowaficha wanawanyanyasa kisaklojia’’. Alisema  Jacob.

Alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa majengo hali inayopelekea watoto wengi kukosa nafasi za masomo, uzio, umeme, usafiri wa kwa wanafunzi pamoja na uhaba wa walimu.

Hata hivyo aliiomba Serikali kuwaandaa walimu kwa kuwapa elimu maalum kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi wenye ulemavu kwani kuna upungufu wa walimu hao hapa nchini.
Mwalimu Frank Joseph akimfundisha  Mwanafunzi Enock Josia wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Huruma iliyopo Ilemela Mkoani Mwanza namna ya kuandika kwa kutumia mguu.
Mkurugenzi wa shule ya msingi Huruma Andrew Jacob akimvisha kiatu mwanafunzi wa shule hiyo Enock Josia baada ya kumaliza kuandika kwa kutumia mguu.

No comments:

Powered by Blogger.