LIVE STREAM ADS

Header Ads

WARATIBU ELIMU MSALALA MKOANI SHINYANGA WAONYWA KUTUMIA PIKIPIKI WALIZOPEWA KISIASA.

Na:Shaban Njia
Serikali katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga imetoa onyo kali kwa waratibu Elimu wa Kata za Halmashauri ya Msalala kutumia pikipiki walizopewa katika shughuli za Kisiasa.

Onyo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya wakati akikabidhi jumla ya pikipiki 16 kwa waratibu Elimu hao ambapo aliwataka pikipiki hizo kutozitumia kwenye siasa na kusema pikipiki hizo zimetolewa mahususi kwa kurahisisha shughuli za Elimu.

Pia Mpesya aliwataka waratibu Elimu hao kutumia taaluma yao kama wasomi na kutobabaishwa na wanasiasa wanaodai kuwa wanatumia siasa kubadilisha hali ya uchumi hivyo wachukue muda mwingi kuisaidia serikali katika uboreshaji wa Elimu.

Mkuu huyo wa Wilaya pia aliwataka waratibu hao kutozitumia pikipiki hizo katika starehe mbalimbali na kuzitumia katika shughuli zisizo kusudiwa na badara yake wazitumie katika shughuli zililizokusudiwa.

“Mkurugenzi hakikisha unatoa fedha kwaajili ya kuzihudumia pikipiki hizi, wape mafuta pamoja na matengenezo madogomadogo halmashauri haiwezi kushindwa kuwasaidia hawa watu muhimu,cha msingi wasizipeleke kwenye starehe wazitumie kwa shughuli hiyo ya kuhudumia watoto,”alisema Mpesya.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Patrick Karangwa alimhakikishia mkuu huyo wa wilaya ya Kahama kuwa katika pikipiki hizo 16 zailizotolewa kwa waratibu elimu kata atahakikisha anazihudumia,na kusema kuwa kati ya kata 18 za halmashauri hiyo ni kata mbili tu ambazo wataendelea kutumia za zamani wakati nao wanatafutiwa.

Hata hivyo mmoja wa waratibu elimu  hao Zachari Sammuel alisema kuwa watahakikisha wanatumia pikipiki hizo kwa shughuli zilizokusudiwa na kusema kuwa kamwe hawatajihusisha na mpango wa siasa.

No comments:

Powered by Blogger.