LIVE STREAM ADS

Header Ads

JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LASHIRIKI MAONYESHO YA BIASHARA YA AFRIKA MASHARIKI.

Kwa mara ya Kwanza Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kitengo cha Usalama Barabarani limeshiriki Maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika Viwanja wa Chuo cha Dar es salaam Institute of Technology Tawi la Mwanza vilivyopo Katika Manispaa ya Ilemela.
Na:George GB Pazzo
Pichani ni Afisa Usalama barabarani ambae pia ni Mratibu wa Elimu kutoka Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza PC Dismas Temba akitoa elimu ya usalama barabarani hii leo kwa wananchi waliotembelea banda la jeshi hilo lililopo katika maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki ambayo huandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini TCCIA.
 Afisa Usalama barabarani ambae pia ni Mratibu wa Elimu kutoka Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kitengo cha Usalama barabarani PC Dismas Temba akitoa maelekezo ya namna kifaa cha kupimia mwendo kasi wa magari barabarani kinavyofanya kazi kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la jeshi la polisi katika Maenyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Viawanja wa Chuo cha Dar es salaam Institute Of Technology Tawi la Mwanza vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela.
Kulia ni Afisa Usalama barabarani ambae pia ni Mratibu wa Elimu kutoka Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kitengo cha Usalama barabarani PC Dismas Temba akiwa na kifaa. PC Temba amewasihi wananchi kufika katika banda hilo ili kupata elimu ya usalama barabarani.
Afisa Usalama barabarani ambae pia ni Mratibu wa Elimu kutoka Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza PC Dismas Temba akitoa elimu ya usalama barabarani kwa wananchi waliotembelea banda la jeshi hilo lililopo katika maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki ambayo huandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini TCCIA.

Maonyesho hayo yalianza Agosti 28 wiki iliyopita na yanatarajia kufikia tamati Septemba Nane mwaka huu ambapo lengo lake ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa nchi za Afrika Mashariki kutangaza bidhaa zao pamoja na kupata fursa ya kubadilishana uzoefu wa kibiashara.

No comments:

Powered by Blogger.