MWAMKO WA KUTEMBELEA MAONYESHO YA BIASHARA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI MWANZA WAPUNGUA.
Baadhi ya Wanachi wakihudumiwa katika banda la Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel katika Maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika Viwanja vya DIT Ilemela Mkoani Mwanza.
Na:George GB Pazzo
Wakazi Mkoani Mwanza wamekuwa na Mwamko mdogo
wa kutembelea Maonyesho ya kumi ya Kibiashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika
katika Viwanja vya Chuo cha Dar es salaam Institute of Technology DIT tawi la
Mwanza vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela.
Baadhi ya Washiriki wa Maonyesho hayo
waliozungumza na Radio Metro hii leo wamewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi
ili kutembelea Maonyesho hayo ambayo yamesheheni bidhaa mbalimbali kutoka ndani
na nje ya nchi kwa ajili ya kunufaika na bidhaa zilizopo pamoja na elimu ya
namna bidhaa hizo zinavyotengenezwa.
Wameongeza kuwa licha ya maonyesho hayo
kuboreshwa mwaka huu ikilinganishwa na miaka iliyopita, bado suala la kiingilio
ambacho ni shilingi elfu moja kwa kila mwananchi anaeyatembelea ni miongoni mwa
sababu zinazosababisha mwamko huo kupungua.
Juhudi za kuwatafuta waandaaji wa Maonyesho hayo ili kuyazungumzia bado zinaendelea baada ya hii leo kugonga mwamba.
Maonyesho hayo yalianza Agosti 28 wiki
iliyopita na yanatarajia kufikia tamati Septemba Nane mwaka huu ambapo lengo
lake ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa nchi za Afrika Mashariki kutangaza
bidhaa zao pamoja na kupata fursa ya kubadilishana uzoefu wa kibiashara.
Agness Emmanuel ambae ni Wakala wa Airtel akizungumza na Radio Metro katika nanda la kampuni hiyo akiwahimiza wananchi kutembelea maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki.
Charles Emmanuel ambae ni Wakala wa Airtel akizungumza na Radio Metro katika nanda la kampuni hiyo akiwahimiza wananchi kutembelea maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki.
Antonia Mchome ambae ni Afisa Mauzo na Masoko akizungumza na Radio Metro katika banda la kampuni ya Tanganyika Instant Cofee akiwahimiza wananchi kutembelea maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki.
Banda la Tanganyika Instant Coffee na wafanyakazi wake
Winnie Alex Chibula kutoka Mtwara akiwa katika banda lake la Dachi Stock Cold linalouza vyombo vya majumbani
Hili ni banda la Crown Paint
Kampuni ya Ving'amuzi ya StarTimes pia inashiriki Maonyesho hayo na wanatoa huduma mbalimbali kwa ofa maalumu
Kampuni ya Ving'amuzi ya Dstv nayo pia inashiriki Maonyesho hayo
Hili ni Banda la Urembo la Ally Captain kutoka Jijini Dar es salaam
BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUIJUZE JAMII
No comments: