LIVE STREAM ADS

Header Ads

HIVI KESHO HUWA INAFIKA KWELI? SOMA HAPA KUFAHAMU ZAIDI.

Kati ya vitu ambavyo Mungu kampa mwanadamu cha thamani na hatakiwi kukichezea ni muda kimojawapo. Ukiwa na tabia ya kuchezea muda wako basi jua mafanikio kwako yatakuwa ni ndoto. 
Watu waliofanikiwa wanafahamu hili na huwa wanajua kabisa kama wakitumia muda wao vibaya basi hakuna namna nyingine ambayo wanaweza kurudisha mda nyuma, ukipoteza masaa mawili unapiga umbea ujue ndio hakuna namna ya kuyarudisha tena katika maisha yako.
Siku ya leo ni nzuri sana kwako na ni zawadi kutoka kwa Mungu kwenye maisha yako, siku ya kesho itakuwa ni hadithi za kusadikika stori za kuongea hakuna anaejua kesho yake itakuwaje.
Hutakiwi kwenye maisha yako kuwa na tabia ya kusema nitaanza kufanya kesho na ukaacha kuanza kufanya leo hii ni kwa sababu kesho huwa haifiki ikifika kesho utasema kesho hivyo hivyo badala ya kusema kesho sema tarehe,mwezi, mwaka na muda.
Saa zingine tujifunze vitu kwenye mazingira tunayoishi ukienda kukata tiketi ya kusafiri iwe ya nde, gari au meli huwa unaulizwa siku tarehe na sehemu unakuelekea hivyo badala ya kuishi kwenye ulimwengu wa kesho be definate.
Yaani sasa hivi (namaanisha leo)ni rahisi kuanzisha biashara kuliko kipindi kingine chochote kile kwenye historia na mtu pekee anaekuzuia usianzishe biashara yako sasa hivi ni wewe, sasa hivi kuna maendeleo ya teknolojia kubwa katika masuala ya mtandao ambayo unaweza kuitumia kutangaza biashara yako ikiwa utaitumia mitandao ya kijamii vizuri badala ya kuweka picha za wik-end hii ulikuwa wapi.
Jua tu hakuna mtu wa kukusukuma hata sisi Life secrets hatuwezi ni jukumu lako wewe mwenyewe unataka badilisha maisha yako siku ya leo badili mambo unayofanya jifunze na anza kufanya mambo mengine.
Niseme hivi Bob aliwahi kusema The main thing is to keep the main thing the main thing. What is the main thing? The main thing is time and money freedom(kitu cha msingi ni kuweka kitu cha msingi kuwa cha msingi. Kitu cha msingi ni Muda na Uhuru wa kifedha) utashangaa namna utakavyokuwa na muda mwingi kama utakuwa hufikiri kuhusu fedha.
Ni siku hii ya leo inakupa kitu cha kuongea siku ya kesho sasa kama siku ya leo hujafanya chochote ambacho utakiongea kesho je kesho yako itakuwaje? Tumia vizuri siku ya leo ili siku ya kesho uwe na cha kuongea. Usijifunge katika siku ya kesho leo ndio siku ya pekee ya kufanya na fanya kwa jitihada zako zote.
SHEA UJUMBE HUU NA RAFIKI ZAKO WENYE TABIA YA KUSEMA KESHO NA HAWAPO DEFINATE.
Whatsup us @0689 452 670
Kumbuka darasa awamu ya pili kwa wale wanaopenda kupata madini ya nguvu ya kuwafanikisha kimaisha litaanza tarehe 14/09/2015 anza kujiandikisha mapema wiki ya kwanza unasoma bure unapata audio na maandishi.
email us @allnhumph@gmail.com

No comments:

Powered by Blogger.