BINAGI RADIO: KUMBUKUMBU YA MAUAJI YA MWANAHABARI DAUDI MWANGOSI KUFANYIKA KESHO.
Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Abubakar Karsan
Na:George GB Pazzo
Muungano
wa Vyama vya Waandishi wa Habari nchini UTPC unatarajia kuadhimisha Kumbukumbu
ya kumuenzi Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi alieuawa na polisi miaka mitatu
iliyopita kwenye Mkutano wa Kisiasa akiwa kazini katika Kijiji cha Nyololo
Mkoani Iringa.
Hayo yalielezwa wikendi iliyopita na Mkurugenzi Mtendaji wa
Muungano huo Abubakar Karsan wakati akizungumza na Waandishi wa Habri katika
ofisi za Umoja huo zilizopo Isamilo Jijini Mwanza.
Karsan alisema kuwa kumbukumbu hiyo inatarajiwa
kuadhimishwa Septemba mbili mwaka huu Jijini Dar es salaam, ikiwa ni tarehe
ambayo Mwangosi aliuawa.
Alibainisha kuwa katika kuadhimisha Kumbukumbu hiyo, masuala
mbalimbali yanatarajiwa kujadiliwa ikiwemo Usalama kwa Waandishi wa habari
katika kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini pamoja na kutoa taarifa juu ya Mfuko wa
maendeleo wa Daudi Mwangosi Media
Support Fund ambao husimamia tuzo ya Uandishi wa Habari uliotukuka kwa
mwandishi aliejitolea kufanya kazi zake kwa bidii ama kudhurika kutokana na
kazi hizo.
Katika hatua nyingine Karsan aliwaasa Waandishi
wa Habari nchini kutumia vema wajibu wao katika kipindi hiki cha kuelekea
katika Uchaguzi Mkuu na kujiepusha na suala la upendeleo wa wagombea na vyama vya siasa katika kuandika na kuripoti habari za uchaguzi pamoja na kuwachagulia Wananchi viongozi badala
ya kuwaacha wananchi wenyewe wawachague viongozi wanaowata kupitia sanduku la
kupigia kura siku ya uchaguzi mkuu ambao unatarajia kufanyika octoba 25 mwaka
huu.
Daudi Mwangosi aliuawa Septemba Mbili mwaka 2012
na kitu kilichosadikika kuwa ni bovu wakati polisi wakizuia kufanyika kwa
mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema katika Kijiji
cha Nyololo Mkoani Iringa ambapo hadi mauti yanamkuta alikuwa ni Mwandishi wa
Habari wa Kituo cha Runinga cha Chanel Ten na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi
wa Habari Mkoani Iringa.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA
Daudi Mwangosi Enzi za Uhai Wake
No comments: