LIVE STREAM ADS

Header Ads

BENKI YA BARODA YAKABIDHI MADAWATI SHULE YA MSINGI LAKE B, MWANZA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Benki ya Baroda (Bank of Baroda- Tanzania Ltd) imekabidhi msaada wa madawati katika Shule ya Msingi Lake B iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mwanza, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha mazingira ya elimu nchini.

Akizungumza Ijumaa Oktoba 24, 2025 wakati wa zoezi la kukabidhi madawati hayo shuleni hapo, Meneja wa Benki ya Baroda Tawi la Mwanza, Victoria Kavishe alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa ombi lililotolewa na uongozi wa Shule hiyo wakati wa mahafali ya darasa la saba mwaka huu 2025.

Kavishe alisema Benki ya Baroda imekabidhi jumla ya madawati 30 yenye thamani ya shilingi milioni mbili huku akiahidi benki hiyo kuendelea kushirikiana na uongozi wa shule ya msingi Lake B katika kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia shuleni hapo.

"Kwa leo uongozi wa Benki ya Baroda umetoa madawati 30, naamini yatasaidia na kidogo kidogo tutaendelea kumaliza matatizo yaliyopo kwani hatuwezi kuyamaliza siku moja" alisema Kavishe.

Naye Mkuu wa Shule ya Msingi Lake B, Mwl. Emmanuel Edwin alitoa shukurani kwa uongozi wa Benki ya Baroda kwa uaminifu wa kutimiza kwa wakati ahadi waliyoitoa kwa kipindi cha mwezi mmoja na kusema hiyo ni ishara pia ya ufanisi pia wa huduma za kibenki zinazotolewa na benki hiyo.

Nao wanafunzi wa shule ya msingi Lake B walishukuru Benki ya Baroda kwa kuwakabidhi madawati hayo wakisema yatasaidia kuondoa changamoto ya wanafunzi kukaa darasani kwa kubanana na hivyo kufuatilia masomo kwa umakini.
Na George Binagi, BMG Media
Meneja wa Benki ya Baroda Tawi la Mwanza, Victoria Kavishe (kulia), akimkabidhi madawati Mkuu wa Shule ya Msingi Lake B, Mwl. Emmanuel Edwin (kushoto).
Wafanyakazi wa Benki ya Baroda wakiongozwa na Meneja wa benki hiyo tawi la Mwanza, Victoria Kavishe (kulia mbele), wakikabidhi madawati katika Shule ya Msingi Lake B jijini Mwanza.
Meneja wa benki hiyo tawi la Mwanza, Victoria Kavishe akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi madawati katika Shule ya Msingi Lake B jijini Manza.
Mkuu wa Shule ya Msingi Lake B, Mwl. Emmanuel Edwin akitoa shukurani kwa Benki ya Baroda kwa kutoa msaada wa madawati.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lake B wakiimba shairi la shukurani kwa Benki ya Baroda baada ya kukabidhi madawati shuleni hapo.
Madawati 30 yaliyotolewa na Benki ya Baroda katika Shule ya Msingi Lake B iliyopo jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa Benki ya Baroda wakiwa kwenye picha ya pamoja na waalimu wa Shule ya Msingi Lake B iliyopo jijini Mwanza. 
Wafanyakazi wa Benki ya Baroda wakiwa kwenye picha ya pamoja na waalimu wa Shule ya Msingi Lake B iliyopo jijini Mwanza. 
Wafanyakazi wa Benki ya Baroda wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Lake B iliyopo jijini Mwanza. 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lake B iliyopo jijini Mwanza wakifurahia baada ya kupokea madawati kutoka Benki ya Baroda.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lake B iliyopo jijini Mwanza wakifurahia baada ya kupokea madawati kutoka Benki ya Baroda.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lake B iliyopo jijini Mwanza wakifurahia baada ya kupokea madawati kutoka Benki ya Baroda.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lake B iliyopo jijini Mwanza wakifurahia baada ya kupokea madawati kutoka Benki ya Baroda.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lake B iliyopo jijini Mwanza wakifurahia na mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya Baroda baada ya kupokea madawati.
BARODA ni benki ya kimataifa kutoka India ambayo ilianza kutoa huduma za kifedha Tanzania tangu mwaka 2004 ikihudumia wateja wadogo, wa kati na wakubwa.

No comments:

Powered by Blogger.