LIVE STREAM ADS

Header Ads

SKAUTI KATIKA MANISPAA YA KAHAMA MKOANI SHINYANGA WALALAMIKA KUTELEKEZWA.

Na:Shaban Njia
Kikundi cha umoja wa vijana wa Skauti Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wameeleza kusahaulika kwa Serikali hasa pale wanapokabiliwa na changamoto lukuki zinazotakiwa kutatuliwa na serikali katika kukiendeleza kikundi chao na badala yake wazazi ndiyo wanaojitolea kuwasaidia.

Malalamiko hayo yalitolewa jana na Kamishna wa Skauti Mkoa wa Shinyanga Musa Chama wakati akizungumza na wazazi wa watoto walioko katika umoja huo katika hafra fupi ya Uzinduzi wa Club yao iliyofanyika wilayani Kahama.

Kamishina huyo aliitupia lawama Serikali kwa kushindwa kulijali kundi hilo muhimu ambalo limekuwa likionekana ni kundi muhimu hasa katika Shughuli muhimu za Kitaifa hususani Mwenge wa Uhuru na kuongeza kuwa mara baada ya kupita husahaulika.

Chama aliwaeleza wazazi hao kuwa Serikali wilayani Kahama haina msaada wowote juu kundi hilo hasa kipindi wanapoombwa kufadhili shughuli zao ama misafara mbalimbali ya mafunzo ya watoto hao na na badala yake wazazi hao ndiyowamekuwa msaada mkubwa kwa watoto wao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Skauti Wilaya ya Kahama Mashaka Msekwa ameiomba serikali kuongeza juhudi katika kuwahudumia watoto hao ili kuwapunguzia mzigo wazazi kwani chombo hicho kipo kwa manufaa ya Serikali.

Awali mmoja wa vijana hao Faraja Isack aliwaeleza wazazi kuwa wanakabiiwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhafifu wa miundombinu ya vifaa vya kazi kama mavazi na kukosa misaada mbalimbali, ukosefu wa wafadhili,ukosefu wa usafiri wanapohitaji kusafiri kwenda nje ya Kahama pamoja vifaa vingine.

Hata hivyo mmoja wa wazazi walio hudhulia hafra hiyo fupi Chacha Marwa aliwaomba wazazi kuwasaidia pale wanapobidi kwani fani waliyonayo si uhuni jambo ambalo huenda ndiyo sababu ya serikali kutoelekeza nguvu zao katika kundi hilo na kusema kuwa watoto hao wanajifunza maadili ya Jeshi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kahama Felix Kimaryo alilitaka kundi hilo kutokata tamaa kwa kuwa serikali itahakikisha inaimarisha ushirikiano wake miongoni mwao. 

No comments:

Powered by Blogger.