LIVE STREAM ADS

Header Ads

JIEPUSHE NA MAMBO YAFUATAYO ILI UWE SALAMA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII.

Na:Binagi Media Group
Ni Septemba Mosi Mwaka huu ile Sheria ya Makosa ya Mitandaoni ya mwaka 2015 inatarajiwa kuanza kutumika. 

Huku Sheria hiyo ikiwa inatarajiwa kutumika, wapo wanaosema itasaidia katika maadili ya watumiaji wa mitandao na wengine wakisema itawakandamiza watumiaji wake.

Sasa ili kuwa upande salama, yafuatayo ni mambo kumi unayopaswa kuyaepuka ili kuwa upande huo ambao ni salama kama mtumiaji wa mitandao ya kijamii.

1.Epuka Kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii yetu kupitia mitandao

2.Epuka Kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza kupelekea kuvuruga amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao

3.Epuka Kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadili kwa jamii kupitia mitandao mbalimbali ( Whatsapp,Facebook,Youtube,Inst agram n.k

4.Epuka Kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya kijamii

5.Epuka Kushiriki kusambaza chochote kati ya vilivyotajwa hapo juu ( kutuma kama ulivyopokea ) itakugharimu

6.Epuka Wizi kupitia mitandao mbalimbali na mitandao ya simu utakugharimu

7.Epuka Kumpatia mtu line yako ya simu na kutumika kufanyia wizi ama utapeli itakugharimu.

8.Epuka Kushiriki kumchafua mtu,taasisi,kikundi cha watu kwa namna yoyote kupitia mitandao pia itakugharimu.

9.Epuka Kupoteza simu bila kutoa taarifa na kufunga mawasiliano hayo yanaweza kupelekea kutumika kufanya uhalifu na ukaangukia hatarini.

10.Epuka Kutumia mtandao kwa utapeli kupitia 'brand' ama jina la mtu itakugharimu.

Hukumu: Ni kifungo cha miaka kadhaa gerezani ama faini ya fedha isiyopungua milioni 5 kulingana na kosa lililofanyika.

No comments:

Powered by Blogger.