LIVE STREAM ADS

Header Ads

MLIPUKO WA JENERETA WASABABISHA MALORI YA MAFUTA KUWAKA MOTO JIJINI MWANZA.

Mlipuko wa Jenereta katika Kituo cha Mafuta Kiitwacho SASA KAZI kilichopo katika eneo la Mkuyuni Jijini Mwanza umesababisha Malori Mawili ya Mafuta na pikipiki moja ya mteja kuwaka moto hii.
Na:George GB Pazzo
Kwa Mujibu wa Kamanda wa Zima Moto Mkoa wa Mwanza Andrew James Mbate, tukio hilo limetokea majira ya saa tano asubuhi hii leo.

Amsesema hakuna mtu yeyote aliepata madhara kutokana na mlipuko huo ambao imeelezwa kuwa umetokea wakati wafanyakazi wa kituo hicho wakitoa mafuta katika Lori lililokuwepo Kituoni hapo.

Meneja wa Kituo hicho Charles Philipo Mzatula amesema kuwa bado thamani ya hasara iliyosababishwa na moto huo haijafahamika ambapo amelishukuru jeshi la Zima Moto kwa kusaidia katika zoezi la Kuzima moto huo na hivyo kuepuka madhara makubwa zaidi.
Askari wa Zima Moto wakiendelea na zoezi la Kuzima Moto  katika Kituo cha Mafuta Sasa Kazi kilichopo Mkuyuni Jijini Mwanza. Moto huo umesababisha Malori Mawili kuwaka Moto pamoja na Pikipiki ya Mmoja wa wateja waliokuwa wakipata huduma kituoni hapo.
Mashine katika eneo la Kuwekea Mafuta ya Taa nayo iliwaka moto
Malori yaliyowaka moto ni Scania T 509 AFD lililokuwa na Mafuta aina ya Dizel lita 35,000 ambalo tank lake la mafuta halikulipuka moto na la pili ni T 674 AIU pia Scania.
Miongoni Mwa Lori Lililowaka Moto
Askari wa Zima Moto wakiwajibika kituoni hapo
Askari wa Zima Moto wakiwajibika kituoni hapo
Kamanda wa Zima Moto Mkoa wa Mwanza Andrew James Mbate akizungumza katika eneo la tukio
Kamanda wa Zima Moto Mkoa wa Mwanza Andrew James Mbate akizungumza na wanahabari katika eneo la tukio
Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii

No comments:

Powered by Blogger.