LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MKOANI MWANZA CHAZINDUA RASMI KAMPENI ZAKE ZA UCHAGUZI MKUU.

Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza leo Agost 26, 2015 Kimezindua Rasmi harakati zake za Kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Octoba 25 kwa ajili ya Kuwapata Viongozi katika nafasi za Udiwani, Ubunge na nafasi ya Urais.

Kampeni hizo zimezinduliwa na Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma Livingstone Joseph Lusinde maarufu kwa jina la Kibajaji katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza.

Katika Uzinduzi huo, Lusinde amewahimiza Wananchi na Makada wa CCM kujitokeza kwa wingi katika Mikutano ya CCM ili kuwasikiliza wagombea wake wakiwaeleza namna watakavyowatumikia pindi watakapowachagua.

Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu amewataka Wananchi kukichagua kwa nafasi zote za uongozi ili kiweze kuwatumikia kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Picha zote zinaonyesha mamia ya Wananchi na Makada wa CCM waliohudhuria Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za chama hicho.
Na:Binagi Media Group
Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma Joseph Lusinde maarufu kwa jina la Kibajaji akihutubia katika Mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CCM Mkoa wa Mwanza.
Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii

No comments:

Powered by Blogger.