LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA ACACIA YALALAMIKIWA KATIKA WILAYA YA KAHAMA MKOANI SHINYANGA.

Na:Shaban Njia
Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imeilalamikia Kampuni ya ACACIA kupitia Mgodi wake wa Dhahabu wa Bulyanhulu kutoishirikisha Ofisi hiyo katika mambo mbalimbali hususani majanga  kama lile ya uvujaji wa sumu kutoka katika moja ya mabwawa ya mgodi huo na kuingia katika maeneo wanaoishi Wananchi.

Akizungumza juzi na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Afisa Madini Mkazi wa Wilaya ya Kahama Sophia Omary alisema kuwa ofisi yake imekuwa haishirikishwi katika mambo mbalimbali yanayotokea katika mgodi huo,huku akitolea mfano janga lililotokea mwezi wa tatu mwaka huu ambapo mabwawa ya kuhifadhi sumu ya SYNED yaliyovuja na kutiririsha sumu hiyo kutoka eneo la mgodi na kuingia kijiji cha namba tisa na kusababisha uharibifu wa mazao,vyanzo vya maji na maeneo ya malisho.

“Mimi kama ofisi sikuwa na taarifa yoyote ya kupasuka kwa bwawa lenye kemikali ya SYNED kama imeingia katika eneo la kijiji cha namba tisa na kupelekia kuathiri mali mbalimbali za wananchi ikiwemo mazao kukauka pamoja na vyanzo vya maji vilivyokuwepo kubadilika rangi na hivyo kupelekea wananchi wa kijiji hicho kuwa na hofu ya maisha yao”alisema Sophia Omary.

Kwa upande wake Mkaguzi wa Migodi na Baruti kutoka Wizara ya Madini na Nishati Sabai Nyansiri alisema kuwa kutokana na kutokea kwa tukio hilo Ofisi ya Madini ilikaa kikao na watu wa Mgodi na kufikia mwafaka wa kuwaondoa wananchi wa kijiji cha namba tisa ikiwa ni sambamba na kuwalipa fidia katika maeneo yao waliyokuwa wakiyatumia hapo awali.

No comments:

Powered by Blogger.