LIVE STREAM ADS

Header Ads

WALICHOKISEMA MAKOCHA WA TOTO YA MWANZA NA STAND YA SHINYANGA BAADA YA MCHEZO WA KIRAFIKI.

Na:Oscar Mihayo
Klabu ya Toto Africans ya jijini Mwanza imelazimishwa sale ya bao 1-1 na timu ya Stand united ya mjini shinyanga katika pambano la mechi ya kirafiki kama maandalizi ya kuekekea ligi Kuu Tanzania Bara ya septemba 12 mwaka huu.

Mechi hiyo iliyopigwa katika dimba la CCM Kirumba juzi jijini hapa ilikuwa ya vuta ni kuvute kufuatia kila timu kuonyesha usajili mpya na  kutoa onyo kwa timu shiriki za ligi hiyo.

Kipindi cha kwanza milango ilikuwa migumu lakini dakika ya 2 ya kipindi cha pili Stand United ilijipatia bao la kuongoza kupitia kwa Kassim Banda bao ambalo halikudumu kwani dakika 5 badae Toto ilisawazisha kupitia kwa Japhet Vedastus hadi mwisho wa mchezo ubao ulisomeka 1-1.

Kocha wa Toto Martin Grelics mara baada ya mchezo alisema kuwa kwa sasa timu inaendelea kuimarika katika safu ya ulinzi na kiungo huku akikiri kuwa bado safu ya ushambuliaji haijaimarika vyema.

Aidha aliongeza kuwa kwa sasa ataedelea kujifua na  mechi za kirafiki zaidi ili wachezaji waelewane vizuri kabla ya kuanza kwa ligi na kuongeza kuwa siku ya Ijuma ya wiki hii anatarajia kucheza na timu ya mchangani  ili kujiimalisha zaidi.

Kwa upande wake kocha wa Standi united ambaye pia alikuwa kocha wa zamani wa Simba Patric Leywig alisema kuwa timu yake imecheza chini ya kiwango na kuahidi kulishughulikia tatizo hilo kabla ya kuanza kwa ligi Kuu na kuongeza kuwa lengo kubwa la timu hiyo ni kumaliza na nafasi nne za juu.

No comments:

Powered by Blogger.