Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii zatoa elimu ya utalii kwa wanafunzi Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza program ya kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo jijini Mwanza, kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu utalii wa ndani, uhifadhi na utunzaji wa mazingira.
Programu hiyo endelevu ilianza Jumatano Julai 30, 2025 ikijumuisha taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo ni Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT).
Akizungumza Alhamisi Julai 31, 2025 wakati wa utoaji elimu kwa wanafunzi na waalimu katika shule za Sekondari Nyabulogoya na Mkuyuni jijini Mwanza, Mkuu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua alisema program hiyo itasaidia kutangaza vivutio vya utalii na hivyo kongeza hamasa ya utalii wa ndani nchini.
“Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ina dhamana ya kutangaza utalii wa nchi yetu hivyo programu hii ni mojawapo ya mkakati wa kutoa elimu ya utalii kwa wanafunzi na walimu ili kuhamasisha utalii wa ndani kwa lengo la kuongeza ushiriki wa kundi hilo kwenye masuala ya utalii, kuongeza idadi ya watalii wa ndani pamoja na mapato yatokanayo na utalii” alisema Kabarua.
Naye Mkuu wa Kanda, Idara ya Utalii Kanda ya Ziwa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Martin Mrema alisema ni jukumu la wizara hiyo kutoa elimu kuhusu masuala ya maliasili, malikale na utalii hivyo matarajio ni progamu hiyo kuongeza hamasa ya utalii wa ndani huku wanafunzi wakihamasisha kujiunga na masomo ya uhifadhi na utalii katika vyuo mbalimbali ikiwemo Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT).
Kwa upande wake Afisa Wanyamapori TAWA Pasiansi, Loiruck Moses alisema program hiyo pia inajenga uelewa wa kutambua utofauti wa shughuli za utalii zinazofanyika katika mapori ya akiba ambazo ni pamoja na uwindaji wa wanyamapori tofauti na kwenye hifadhi za Taifa ambapo shughuli hizo haziruhusiwi.
Nao baadhi ya wanafunzi akiwemo Mariam Benjamin na Joseph Jimmy walisema programu hiyo imewasaidia kutambua majukumu ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, umuhimu wa utalii wa ndani pamoja na hatua za kuchukua ikiwemo kuwasiliana na mamlaka husika pindi wanyama wakali kama mamba na tembo wanapoingia katika makazi ya binadamu.
Kupitia program hiyo, pia imetolewa elimu kwa waalimu kuhusu namna ya kuratibu safari za wanafunzi kutembelea vivutio vya utalii kwa makundi kwa lengo la kupunguza gharama za safari na viingilio.
Mkuu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua akitoa elimu ya utalii kwa wanafunzi jijini Mwanza.
Mkuu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua akitoa elimu ya utalii kwa wanafunzi jijini Mwanza.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Nyabulogoya (kushoto) wakimsikiliza mwakilishi kutoka TANAPA.
Afisa Wanyamapori TAWA Pasiansi, Loiruck Moses (kushoto) akieleza majukumu ya TAWA katika uhifadhi na utalii nchini.
Mkuu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua (kushoto) akikabidhi majarida ya utalii kwa wanafunzi.

Mkuu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua (kushoto) akitoa elimu ya utalii na uhifadhi kwa wanafunzi.
Wanafunzi wakisoma jarida la utalii.
Wanafunzi wakisoma jarida la utalii.
Mkuu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua (kulia) akitoa elimu kwa wanafunzi.
Wanafunzi wakifuatilia elimu ya utalii na uhifadhi.
Wanafunzi wakifuatilia elimu ya utalii na uhifadhi.
Mkuu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua (kulia) akimkabidhi mwanafunzi jarida la utalii.
Mwalimu Jusi Leonard kutoka shule ya sekondari Bulogoya akitoa shukurani kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia taasisi zake kwa kutoa elimu ya utalii na uhifadhi katika shule za msingi, sekondari na vyuo.
Wanafunzi wakifuatilia elimu ya utalii na uhifadhi.
Wanafunzi shule ya sekondari Mkuyuni wakifuatilia elimu ya utalii na uhifadhi.
Mkuu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua akitoa elimu kwa wanafunzi.
Mwakilishi kutoka TANAPA kutoka Kisiwa cha Saanane akitoa elimu kwa wanafunzi.
Mwakilishi kutoa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) akihamasisha wanafunzi kujiunga na chuo hicho baada ya kuhitimu kidato cha nne ili kupata ujuzi zaidi kuhusu masuala ya utalii na uhifadhi.
Afisa Wanyamapori TAWA Pasiansi, Loiruck Moses akitoa elimu kwa wanafunzi.
Afisa Wanyamapori TAWA Pasiansi, Loiruck Moses akizungumza na wanafunzi.
Afisa Wanyamapori TAWA Pasiansi, Loiruck Moses akizungumza na wanafunzi.
Mwakilishi kutoka TANAPA kutoka Kisiwa cha Saanane akitoa elimu kwa wanafunzi.
Mkuu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua (kushoto) akifafanua jambo.
Mkuu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua (kulia) akikabidhi jarida la utalii kwa mwanafunzi.
Mkuu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua (kulia) akikabidhi jarida la utalii kwa mwanafunzi.
PIA>>> BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI
No comments: