LIVE STREAM ADS

Header Ads

KESI YA MAUAJI INAYOMKABIRI MKURUGENZI WA MABASI YA J4 YATAJWA. SOMA MAAMUZI YAKE.

Waandishi wa Habari Jijini Mwanza wakiwajibika Mahakamani.
Na:Binagi Media Group
Kesi ya Mauaji inayomkabiri Mkurugenzi wa Mabasi ya J4 yanayofanya Safari zake katika Mikoa ya Mwanza na Mara Juma Mahende mwenye umri wa miaka 45, kwa mara ya tatu hii leo imetajwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kanda ya Mwanza.

Mahende anakabiliwa na kesi ya kutumia bastola kutekeleza mauaji ya watu wawili Jijini Mwanza ambao ni Ally Mohamed mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Igoma na Cloud Steven mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa Nyasaka baada ya kutokea marumbano miongoni mwao julai 14 mwaka huu majira ya saa usiku katika eneo la Buzuruga.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali Subira Mwandama aliiambia Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na utawasilishwa pindi utakapokamilika.

Hakimu Mfawidhi Mkoa wa Mwanza Wilbert Chuma aliiahirisha kesi hiyo hadi tarehe 27 mwezi huu itakapotajwa tena ambapo mtuhumiwa huyo amerejeshwa rumande.

No comments:

Powered by Blogger.