LIVE STREAM ADS

Header Ads

KESI YA MAUAJI INAYOMKABIRI MKURUGENZI WA MABASI YA J4 YAENDELEA KUUNGURUMA JIJINI MWANZA.

Na:Binagi Media Group
Kesi ya Mauaji inayomkabiri Mkurugenzi wa Mabasi ya J4 yanayofanya Safari zake katika Mikoa ya Mwanza na Mara Juma Mahende mwenye umri wa miaka 45, leo imetajwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza.

Mahende amefikishwa Mahakamani hapo ikiwa ni mara ya nne na tuhuma zinazomkabiri za kutumia bastola kutekeleza mauaji ya watu wawili Jijini Mwanza ambao ni Ally Mohamed mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Igoma na Cloud Steven mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa Nyasaka yaliyotokea mwao julai 14 mwaka huu majira ya saa usiku katika eneo la Buzuruga baada ya kutokea marumbano miongoni mwao.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali Judith Nyaki ameiambia Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kwamba utawasilishwa Mahakamani hapo pindi utakapokamilika.

Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza Bahati Chitepo ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba tisa mwaka huu  itakapotajwa tena ambapo mtuhumiwa huyo amerejeshwa rumande.

Mahende alifikishwa Mahakamani hapo ikiwa ni mara ya nne na kusomewa mashtaka ya kutumia bastola kutekeleza mauaji ya watu wawili Jijini Mwanza ambao ni Ally Mohamed mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Igoma na Cloud Steven mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa Nyasaka yaliyotokea mwao julai 14 mwaka huu majira ya saa usiku katika eneo la Buzuruga baada ya kutokea marumbano miongoni mwao.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali Judith Nyaki aliiambia Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kwamba utawasilishwa Mahakamani hapo pindi utakapokamilika.

Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza Bahati Chitepo aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba tisa mwaka huu  itakapotajwa tena ambapo mtuhumiwa huyo amerejeshwa rumande.

No comments:

Powered by Blogger.