LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU CCM MKOA WA MWANZA AWATAKA WANANCHI WA NYAMAGANA NA ILEMELA KUTORUDIA MAKOSA TENA.

Judith  Ferdinand
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu amewataka wananchi katika Majimbo yanayoongozwa na upinzani yakiwemo Nyamagana na Ilemela kutorudia makosa katika kuwachagua wawakilishi wao kama walivyofanya mwaka 2010.

Mtaturu aliyasema hayo wakati akihutubia umati wa wananchi waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho Mkoani Mwanza uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mbugani Jijini Mwanza.
“Siasa ni maisha ya watu, tatizo watu wamebaki kufanya ushabiki wa Simba na Yanga katika siasa.Waache ushabiki watafute maisha. Mwaka 2010 Nyamagana na Ilemela mlichagua kwa hasira mkamchagua Wenje Ezekia na Highness Kiwia,si kwamba mlimependa Wenje,”alisema Mtaturu.

Aliwataka wananchi wa majimbo hayo, washushe mizigo hiyo (Wenje na Kiwia) wa Chadema, waichague CCM mwaka huu,kuanzia kwa Rais,Wabunge na Madiwani kwa ajili ya maendeleo yao.

Alidai kuwa mwaka 2010 waliokota mbunge ambaye hakuwa na malengo ya maendeleo kwani anapoulizwa amewafanyia nini wananchi wa Nyamagana anajibu amewajengea ujasiri.

Alisema kitendo hicho kinawadhahlilisha na wakatae kudhalilishwa,wala  wasikubali kuliwa mchana kweupe ili ifikapo Oktoba 25 mwaka huu,wamshikishe adabu kwa kumnyima kura.
 
Mtaturu alimtuhumu Wenje kuwa, alianzisha mfuko wa elimu jimboni humo,lakini akashindwa kuwa mwaminifu akatumia fedha hizo kwa maslahi yake,kati ya hizo fedha Rais Jakaya Kikwete bila kujali chama chake,lakini kwa kujali wananchi wa Nyamagana, alichangia Sh 10 Milioni.
Kwa upande wake mgombea ubunge wa CCM jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula mara baada ya kukabidhiwa ilani ya CCM na kubainisha kuwa anatambua jukumu na uzito wa kazi anayoiomba na kwamba anao uwezo wa kuitumikia.

Mabula alisema “nafahamu watu wa Mwanza wanavyohangaika,kipaumbele changu kitakuwa ni miundombinu kwani Ilani  inazungumzia nyongeza ya barabara.Tutajenga barabara za mawe kwa wananchi wanaoishi kwenye miinuko.Ndio maana naomba ridhaa yenu,msifanye kosa kupiga kura ya ndio kwa wagombea wa vyama vingine zaidi ya CCM kwa nafasi ya urais, ubunge na udiwani”.

Alisema ilani ya uchaguzi ya CCM aliyopokea ataisimamia na kuitekeleza kwa vitendo kwani imebeba mambo mengi ya msingi ikiwemo  sekta ya elimu, afya na miundo mbinu ya barabara.
Alieleza kuwa,atawaunganisha  wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa ili wadogo wainuke wakiwemo machinga,wavuvi na wafanyabiashara wa aina zote,kwa sababu hakuna faida kuwaangalia machinga lazima watengenezewe mazingira ili waheshimiwe na kukopesheka.

Mabula alikana kuvunja matoroli ya wananchi na akadai ni yeye aliyekataa kuwaondoa watu katika maeneo yao wanayofanyia biashara hivyo akichaguliwa atakuwa tayari kusimamia vipaumbele vyake na wakijipanga maendeleo yanaweza kupatikana.

No comments:

Powered by Blogger.