LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKALA "MAFANIKIO SIYO AJALI" SEHEMU YA TATU.

Soma HAPA Sehemu ya Pili Ili Twende Sawa.
Ni lazima uwe na mipango mikubwa katika maisha yako, moja ya sababu ya watu kutokufanikiwa ni kwamba mipango yao ni midogo mno kiasi ambacho hata akimshirikisha mtu anaona mbona ni kawaida sana.

Ukiwa na mipango mikubwa inavutia watu,utakutana na watu wakubwa ambao watatamani kuona namna gani utafanikisha hiyo ndoto yako watakupa msaada wa maarifa, mipangilio,fedha na kadhalika. we hujawahi jiuliza kwa nini benki wapo radhi kumkopesha mtu millioni 100 lakini hawamkopeshi mtu millioni 1?
Baada ya kuwa na mipango yako hiyo mikubwa hakikisha unaiandika usiamini akili yako, sisi kama wataalamu wa Afya na Maendeleo binafsi tunajua kabisa wewe kuandika kitu ni nusu ya kukipata (50%) nusu nyingine ipo katika utendaji.
Jua hivi ni rahisi sana mtu kufanyia kazi kitu alichokiandika chini kwa mkono wake mwenyewe kuliko kile ambacho hajakiandika eeeh ndio maana katika biashara yako ni muhimu kuwa na mpango kazi, utafanyaje hiyo kazi ule unakupa dira ya moja kwa moja namna ambavyo kazi na hiyo biashara yako inavyotakiwa kufanywa kikamilifu usikurupuke kufanya kitu pasipo mpango maana utashindwa kaa chini kwanza panga kisha ndipo utoke ukaanze kufanya.
Lakini pia usije ukapoteza muda mrefu katika kuandika na kupangilia ukasahau kuanza mimi sijui namna ambayo unaweza kumiliki kitu pasipo kukifanyia kazi, ndio mpango mdogo unaotendewa kazi ni bora kuliko mpango mkubwa uliowekwa kwenye makaratasi kabatini ndio hapa lazma nikazie ni lazima uelewe hili sasa usijidai unapangilia mambo kwa miaka 10 pasipo kuanza utapigwa na kitu kinachoitwa hofu ya kuanza na utajikuta unasema hiki kitu hakiwezekani.
Kweli nakuhakikishia usipokuwa na mpango kwenye maisha yako, Ni nini unataka kufanya na utafanyaje nakuhakikishia lazima utatumikia watu wenye mipango hii sio siri ni kitu cha ukweli kabisa, wewe kwenye iyo taasisi unayofanya kazi mwanzoni ilianza kama wazo fulani katika akili ya mtu kisha akalipangilia namna gani atalifanya baada ya hapo akaanza kulifanyia kazi leo hii wewe ni muajiriwa hapo. 
Sasa na wewe fikiri ni namna gani utaanzisha kitu fulani ili watu nao wapate kazi kupitia hicho ulichoanzisha maaana tusikae kulalamika hakuna ajira sasa kama kila mtu analalama kuhusu ajira na anataka kuajiriwa tuu ni nani atamwajiri mwenzie? 
Kijana funguka ona nje ya boksi waza mbali badala ya kufikiri nitaajiriwa wapi fikiri nitaajiri watu wangapi kwa wazo langu nililo nalo sasa usiniambie tatizo ni mtaji tatizo sio mtaji nakuhakikishia labda tu hujajua namna ya kupata mtaji tatizo ni mawazo sahihi na mipango yes hilo ndio tatizo. 
Je una wazo gani zuri na mtaji umekuwa ukikusumbua? Kama unasumbuliwa na mtaji tukuelezee njia 12 ambazo unaweza ukajipatia mtaji.
Lakini pia hilo wazo lako hakikisha ni la kusaidia watu usiwe mchoyo kuwa na tabia ya kusaidia watu wengine ndipo nawe unapobarikiwa eeeeh ndivyo ilivyo na usivune kitu ambacho hujapanda ni dhambi kubwa hata kwa Mungu,usithubutu kwenda kuiba fedha au kitu fulani ambacho sio chako utalaaniwa maana utatenda dhambi na maana ya dhambi ni kuenda kinyume na sheria.
Chunguza utagundua hii dunia inatawaliwa na sheria ni kiasi tuu cha kuzifahamu hizi sheria na kuzitendea kazi, sasa hili ni somo refu sana la sheria na hapa huwa tunakuandikia mambo kwa ufupi sana jua tuu kuna sheria kama ya kupanda na kuvuna,sheria ya kutii, sheria ya kutoa,sheria ya kutokuleta upinzani, sheria ya kuvutia, sheria ya mtetemeko na kadhalika zipo nyingi sasa ni vema kuzifahamu walau hata kwa ufupi inshalah siku tukipata muda tutakufundisha moja moja kwa kifupi zingine mpaka uhudhurie semina zetu au pengine ununue vitabu vidogo tulivyo andika.
Sasa nataka nikuambie ukiwa na mipango dhahiri kufanikiwa kwenye maisha ni rahisi kuliko kutokufanikiwa kwa maana utafanya mengi na kwa umakini kwa kuwa unajua unataka nini na unajua unaelekea wapi mtu asiekuwa na mipango hana tofauti na meli isiyokuwa na dira(uelekeo)atapotea tu na lazima atatumika na wengine waliokuwa na mipango.
LIFE SECRETS COMPANY WANAKUTAKIA SIKU NJEMA. WHATSPIKA NASI 0689 452 670 email us @ allnhum@gmail.com

No comments:

Powered by Blogger.