LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKAMU MWENYEKITI SHIREMA ADAIWA KUWANYANYASA WACHIMABAJI WADOGO MKOANI SHINYANGA.

Na:Shaban Njia
Serikali imeombwa kuingilia kati mgogoro uliopo kati ya wachimbaji wadogo wadogo wa machimbo yaliyopo katika Kata ya Bugarama katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kutokana na Makamu Mwenyekiti wa  Chama cha Wachimbaji wa Madini (SHIREMA) kulalamikiwa kutumia vibaya madaraka yake kujimilikisha eneo la uchimbaji kinyume cha sheria.
Malalamiko hayo yalitolewa na wachimbaji hao wakimshutumu Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Shinyanga Nicodemas Majabe kuwa alivamia moja ya eneo la wachimbaji hao lililopo katika Kijiji cha Igwamanoni na kudai kuwa eneo hilo ni lake na ana leseni  ya kulimiliki kihalali licha ya uongozi wa Kijiji hicho kutomtambua kama mchimbaji halali.
Mmoja wa wachimbaji hao Kinyami Maduhu alisema kuwa mwenyekiti huyo alivamia eneo la Kijiji hicho baada ya kubaini kuwa kuna madini ya dhahabu, ambapo anatuhumiwa kutumia cheo chake kuwafukuza wachimbaji waliokuwepo awali kwa misingi kuwa yeye ndiye kiongozi wao. 
“Hapo awali kutokana na Majabe kujitambulisha kwetu kuwa eneo hilo ni lake tulikubaliana awe anachukuwa mawe, lakini  baada ya shimo hilo kuanza kutoa dhahabu kwa wingi Majabe alitugeuka na kuwaita Polisi kufunga Duara hili ambapo hadi sasa jeshi la Polisi linatumia nguvu kubwa kutufukuza”. Alisema Maduhu.
Akijibu tuhuma hizo Majabe alisema kuwa wachimbaji hao walivamia eneo lake ambalo analimiliki kihalali huku akiwatuhumu wachimbaji hao tuhuma za wizi katika eneo lake la machimbo.

“Mwandishi hizo siyo habari za kweli, hawa ni wezi wakubwa wamevamia mgodi wangu ambao naumiliki kihalali na leseni ninayo, wamechimba dhahabu kwa kuniibia ambapo siku ya kwanza wameiba dhahabu yenye thamani ya shilingi 14 na siku ya pili dhahabu yenye thamani ya shilingi milioni 80, fika eneo la tukioujionee sina mengi zaidi. Alisema Majabe.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Igwamanoni Zuberi Paul alisema kuwa serikali ya kijiji haimtambui kama mchimbaji bali inamtambua kama makamu mwenyekiti wa chama cha kutetea wachimbaji wadodo wadogo(SHIREMA) na kama ni mchimbaji kijiji kingeitambua leseni hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.