LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAONYESHO YA NANE NAE 2015 KANDA YA ZIWA YAFUNGULIWA RASMI. WAANDAAJI WAPEWA RAI.

Na:Malongo Mbeho
WakUlima na Wafugaji kwa kushirikiana na Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Wakulima na Wafugaji Nanenae Kanda ya Ziwa wametakiwa kuandaa maonyesho hayo kwa vitendo ili kutoa fursa kwa wananchi kujifunza zaidi kupitia mfumo wa shamba darasa.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Erasto Mbwire, katika ufunguzi wa maadhimisho hayo yaliyoanza jumamosi iliyopita ya Agosti Mosi katika Viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza yakifanyika Kikanda katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa..

Mbwire alisema kuwa Maonesho ya mwaka huu yamekosa uhalisia wake kutokana na kuwa na maandalizi yasiyo na ufanisi ufanisi na hivyo kupelekea wanaofika katika maonyesho hayo kutojifunza kwa vitendo.

Katika hatua nyingine Mbwire aliwahimiza waandaji wa maonesho hayo kuchukua hatua za haraka ili kujenga majengo ya kudumu ili kuyafanya yawe ya kuvutia zaidi.

Akizungumza na Binagi Media Group, Benedict Saule kutoka banda la Benki Kuu ya Tanzania alisema kuwa Benki hiyo inashiriki katika maonesho hayo ili kupata fursa ya kutoa elimu ya fedha halali za Tanzania na kuwaepusha wananchi na utapeli wa fedha bandia huku akitumia fursa hiyo kukanusha taarifa zinazoenea kuwa kuna madini ya thamani katika sarafu za shilingi 500 na kusema kuwa huo ni upotoshaji kwa watumiaji wake.


Kilele cha Maonyesho ya Siku ya Wakulima na Wafugaji Nane Nane hapa nchini huadhimishwa kila August Nane ya kila mwaka na yaliasisiwa na Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo Kauli Mbiu kwa mwaka huu ni MATOKEO MAKUBWA SASA, TUCHAGUE KIONGOZI BORA KWA KILIMO NA UFUGAJI.
Tazama Picha HAPA

No comments:

Powered by Blogger.