LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIONGOZI WA SERIKALI WAHIMIZWA KUCHUKUA HATUA ILI KUBORESHA MAONYESHO YA NANENANE KANDA YA ZIWA.

Timu ya Masoko na Mauzo kutoka Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania ikimhudumia Mteja aliefika katika Mabanda ya Kampuni hiyo katika Maonyesho ya Wakulima na Wafugaji maarugu kwa jina la Nanenane yanayofanyika kwa Kanda ya Ziwa Viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza.
Judith Ferdinand Mwanza
Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa, wamehimizwa kuchukua hatua ya kuboresha miundombinu ya kudumu ikiwemo kujenga mabanda ya maonyesho katika viwanja vya Nyamongolo Jijini Mwanza yanapofanyika Maonyesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenae Kanda ya Ziwa.

Wito huo ulitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Elaston Mbwiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonyesho ya Nanenane mwaka huu yanayofanyika kwa mara ya tatu mfululizo kwa Kanda ya Ziwa katika Viwanja hivyo.

“Sisi viongozi lazima tujitahidi kuboresha miundombinu na kuboresha maonyesho haya kama kanda nyinge, ni aibu kwa kanda yetu kuwa ya mwisho wakati chimbuko la Nanenane lilianzia kwetu, baada ya wakulima wa pamba kutaka kuwaonyesha wananchi umahiri wao katika kilimo na kuwaelimisha". Alisema Mbwiro.

Pia alisema Viwanja vya Maonyesho ya Nanenae Kanda ya Ziwa vinahitaji kuboreshwa zaidi ambapo aliikumbuka Kampuni ya Tan- Trade kujenga  mabanda na miundombinu ya kudumu katika viwanja hivyo kama ilivyo ahidi mwaka jana katika Maonyesho hayo.

Hata hivyo aliwataka viongozi hao  kutokuwa waandaaji wa maonyesho hayo na badala yake kuwaachia wahusika ambao ni Chama cha Wakulima na Wafugaji,kwaajili ya kuaandaa kwa utalamu zaidi  ili kuleta ufanisi na ushawishi kwa wananchi.

Aliwaomba wadau wanaoshiriki katika maonyesho hayo mwakani wachukue nafasi ya kuwafundisha wananchi namna ya kuendesha ufugaji wa kisasa na wenye tija kubwa.

Kupitia kauli mbiu ya Maonyesho hayo mwaka huu inayosema "Tuchague Viongozi Bora Kwa Maendeleo Ya Kilimo Na Ufugaji", Mbwiro aliwataka wananchi kutunza kadi zao za kupigia kura kwa ajili ya kumchagua kiongozi anayefaa katika uchaguzi Mkuu mwaka huu unaotarajia kufanyika Oktoba 25.

No comments:

Powered by Blogger.