LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKUBWA YAIBUKA KATIKA KANISA LA BABA GODY JIJINI MWANZA.

Na:Binagi Media Group
Waumini wa Kanisa la Throne Of Glory Ministry International Tanzania Maarufu kama Kwa Baba Gody lililopo Jijini Mwanza wameondolewa katika Kanisa hilo chini ya ulinzi wa Polisi kwa amri ya Mahakama baada ya Waumini hao kugoma kutoka katika jengo la kanisa hilo ili kumpisha mmiliki wake kuendelea shughuli zake.

Habari zinaeleza kuwa mmiliki wa jengo hilo ni Mkurugenzi wa Mabasi ya Zubery ambae alitoa jengo hilo kwa muda, kwa ajili ya matumizi ya ibada za kanisa hilo linaloongozwa na Mchungaji anaefahamika kwa jina Nabii Baba Gody Mfalme.

Agizo la Waumini wa kanisa hilo kukabidhi jengo hilo lililopo Mtaa wa Pamba B, Kata ya Pamba lilitolewa kwa mara ya kwanza tarehe 18.07.2015 bila mafanikio, mara ya pili tarehe 03.08.2015 napo bila mafanikio hadi hii leo walipovurushwa kwa nguvu chini ya ulinzi wa polisi kwa kimari cha mahamaka.

Kulizuka mabishano ya hapa na pale kati ya wafanyakazi wa kampuni ya udalali (Action Mart) iliyopewa jukumu la kuondoa mali zilizokuwa katika kanisa hilo dhidi ya waumini wake ambao walikuwa wakidai kuwa wataondoka pindi Mungu wao atakapowaambia hali iliyowalazimu polisi kutumia mabobu ya machozi kutuliza hali hiyo.

Hatimae hali ilitulia na baadae waumini hao wakaanza kuhamisha mali na vitu vilivyokuwa katika jengo la Kanisa hilo na kuvipeleka kusikojulikana huku umati mkubwa uliokuwa ukishuhudia tukio hilo ukitaka kujua baadhi ya mali zilizokuwa katika makabati yaliyotolewa ndani ya jengo hilo.

Wanahabari nusura nao waingie matatani na muumini wa kanisa hilo kila walipokuwa wakijaribu kutekeleza wajibu wao na hakuna hata mmoja aliekuwa tayari kuzungumzia tukio hilo ambapo duru za habari zikidokeza kuwa tukio hilo limetokea huku mchungaji wa kanisa hilo akiwa yuko nje ya nchi.

Mashuhuda wa tukio hilo wamezungumza mambo mengi kuhusiana na Kanisa hilo japo hakuna ushahidi wa moja kwa moja juu ya walichokuwa wakikieleza ikiwemo mrengo wake wa kiimani.

No comments:

Powered by Blogger.