LIVE STREAM ADS

Header Ads

MGOMBEA UDIWANI AAIDI FURSA MBADALA KWA WAKAZI WA KATA YA BULYANHULU MKOANI SHINYANGA.

Na:Shaban Njia
Mgombea Udiwani kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (ccm)Kata ya Bulyanhulu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga John Kiganga amesema kuwa iwapo kama atapata ridhaa ya kuchaguliwa kuwa diwani wa Kata hiyo, atahakikisha anabuni fursa nyingine za ajira badala ya Watu wa eneo hilo kutegemea ajira katika Mgodi wa Bulyanhulu.

Akizungumza na BMG jana, Kiganga alisema kuwa kwa sasa Wananchi wa kata ya Bulyanhulu ambayo ipo jirani na Mgodi  wa Dhahabu wa Bulyanhulu Wananchi wake mara kadhaa wamekuwa katika malumbano makubwa na Mwekezaji wa Mgodi huo kuhusu ajira hali ambayo imepelekea kutokuwa na mahusiano mazuri baina ya pande hizo mbili.

“Kuna fursa nyingi ambazo vijana wanaweza kufanya na zikawa ni moja ya ajira katika katika kata ya Bulyanhulu kama vile ufugaji wa Samaki ambapo tunaweza tukafuga na kuwauzia Wenyewe na kwa muda wa miezi mitatu tuu mtaona mabadiliko makubwa kwa Vijana wa Kata ya Bulyahulu”. Alisema John Kiganga.

Aidha aliwataka Vijana wa Kata hiyo kuacha fikra za kupata ajira katika Mgodi wa Bulyanhulu bali wajikite katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo kama vile ufugaji pamoja na kuunda vikundi mbalimbali vya kuweka na kukopa (SACOS) kwa lengo la kukuza  mitaji yao na kuweza kufanya biashara na Mgodi huo.

“Nikipata ridhaa ya kuongoza Wanachi wa Kata ya Bulyanhulu nitaunda Vikundi vya kuweka na kukopa ili Wanachi waweze kupata fedha angalau kidogo kwa ajili ya kuendesha biashara ndogondogo katika eneo hilo kwa ni wawekezaji hawa wamekuwa wakinunua hata nyama kutoka nchi za nje na huku Wananchi wa eneo hili wanaweza kufanya nao biashara hiyo”, Aliongeza Kiganga.

Mgombea Udiwani huyo aliendelea kusema kuwa katika kata ya Bulyanhulu ni mambo mengi ya kimaendeleo katika kata hiyo ameweza kusadia Wananchi wa eneo hilo kwa muda miaka minne iliyopita katika sekta mbalimbali kama vile Elimu, maji pamoja Kilimo hali ambayo inaweza kuwa chachu ya yeye kuweza kupata ushindi katika uchaguzi wa Udiwani katika kata hiyo kupitia CCM.

No comments:

Powered by Blogger.