LIVE STREAM ADS

Header Ads

MICHUANO YA AIRTEL RISING STAR 2015 YAFUNGULIWA MKOANI MWANZA.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) jana Jumamosi akifungua Michuano ya Soka kwa vijana walio chini ya Umri wa Miaka 17 Airtel Rising Star mwaka 2015 Mkoani Mwanza. 
Konisaga alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo katika ufunguzi huo uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Kwa Mwaka wa Tano Mfululizo, Michuano hiyo imekuwa ikidhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano nchini ya Airtel na imekuwa ikiibua vipaji vya soka kwa vijana nchini.
Na:Binagi Media Group 
Mwenyekiti wa Soka la Vijana kutoka TFF Ayub Nyenzi akizungumza katika Ufunguzi wa Michuano ya Airtel Rising Star 2015 Mkoani Mwanza.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Kanda ya Ziwa Emmanuel Raphael akizungumza katika Ufunguzi wa Michuano ya Airtel Rising Star 2015 Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza MZFA Jackson Manji Songora akizungumza katika Ufunguzi wa Michuano ya Airtel Rising Star 2015 Mkoani Mwanza.
Kutoka Kushoto ni Meneja Masoko wa Aitel Kanda ya Ziwa Emmanuel Raphael, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu), Mwenyekiti wa Soka la Vijana kutoka Chama cha Soka nchini TFF Ayub Nyenzi na wa mwisho ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza Jackson Manji Songora wakiwa katika Uzinduzi wa Michuano ya Soka kwa Vijana walio na Umri chini ya Miaka 17 iitwayo Airtel Rising Star Mkoani Mwanza.
Kutoka Kulia ni Kikosi cha Alliance Sports Academy, Wanafuata waamuzi na Mwishoni ni Kikosi cha Gold Sports Academy. 
Timu hizi ndizo zilivyocheza katika ufunguzi wa Michuano ya Airtel Rising Star 2015 Mkoani Mwanza juzi jumamosi na matokeo yalikuwa Sare Tasa (0-0).
Kutoka Kushoto ni Kikosi cha Alliance Sports Academy, Wanafuata waamuzi na Mwishoni ni Kikosi cha Gold Sports Academy. 
Timu hizi ndizo zilivyocheza katika ufunguzi wa Michuano ya Airtel Rising Star 2015 Mkoani Mwanza juzi jumamosi na matokeo yalikuwa Sare Tasa (0-0).
Kikosi cha Timu ya Alliance Sports Academy kutoka Nyamagana Mkoani Mwanza chini ya Umri wa Miaka 17
Kikosi cha Timu ya Soka ya Gold Sports Academy cha Ilemela Mkoani Mwanza chini ya Umri wa Miaka 17.
Kikosi cha Timu ya Soka ya Gold Sports Academy cha Ilemela Mkoani Mwanza chini ya Umri wa Miaka 17 kikiwa katika Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga na viongozi wengine wa TFF, MZFA na Airtel.
Kikosi cha Alliance Sports Academy  chini ya miaka 17 kikiwa katika Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (Mwenye Kofia) na viongozi wengine wa TFF, MZFA na Airtel.
Waamuzi, Viongozi wa Soka kutoka TFF, MZFA na Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga katika ufunguzi wa Michuano ya Airtel Rising Star 2015 Mkoani Mwanza jana jumamosi.
Mgeni rasmi akikagua kikosi cha Gold Sports Academy 
Mgeni Rasmi akikagua kikosi cha Alliance Sports Academy
Mgeni Rasmi Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza akifungua Michuano ya Airtel Rising Star 2015 Mkoani Mwanza jana jumamosi.
Timu ya Soka ya Gold Sports Academy kutoka Ilemela na Alliance Sports Academy kutoka Nyamagana ziliweza kutoka Sare Tasa (0-0) katika Ufunguzi wa Michuano ya Soka kwa Vijana walio chini ya Umri wa Miaka 17 Mkoani Mwanza. Uzinduzi huo ulifanyika jana Jumamosi katika Uwanja wa CCM Kirumba.

No comments:

Powered by Blogger.