LIVE STREAM ADS

Header Ads

UZINDUZI RASMI WA NMB DEBIT MASTER CARD WAFANA JIJINI MWANZA.

Juzi Ijumaa Bank ya NMB (National Microfinance Bank) ilizindua Rasmi Kadi zake za NMB MASTER CARD Jijini Mwanza. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Nyerere, Gold Crest Hotel na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo wateja wa NMB Bank.

Katika picha ni zoezi la uzinduzi wa Kadi hizo  likifanyika ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Stanslaus Mulongo ambapo aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga.

Card hizo zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni Tanzanite Debit kwa ajili ya Wateja wa kawaida ambayo inayotoa fursa kwa mteja kutoa kiasi cha fedha katika ATM Machine hadi Milioni Moja kwa Siku, Titanium Debit kwa ajili ya wateja wa Kati ambayo hurusu mteja kutoa pesa katika ATM Machine hadi shilingi milioni Tatu kwa siku na World Debit ambayo hurusu mteja kutoa pesa katika ATM Machine hadi shilingi Milioni Tano kwa siku na kadi zote ni salama zaidi kwa ajili ya ulinzi wa pesa za mteja.
Na:Binagi Media Group
Mkurugenzi wa Hazina kutoka Makao Makuu ya NMB Aziz Chacha (Kushoto) akipongezana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) ambae alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo.
Kutoka kushoto ni Warioba Sanya ambae ni Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Mkurugenzi wa Hazina kutoka Makao Makuu ya NMB Aziz Chacha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa Abraham Agustino na Getrude Mallya ambae ni Meneja wa NMB Wateja binafsi.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akizungumza katika Uzinduzi wa NMB Master Card Jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Hazina kutoka Makao Makuu ya NMB Aziz Chacha akizungumza katika uzinduzi Rasmi wa NMB Master Card Jijini Mwanza.
Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa Abraham Agustino akizungumza katika uzinduzi Rasmi wa NMB Master Card Jijini Mwanza.
Meza Kuu
Lulu Jama kutoka Sahara Media Group ndie alikuwa Mshereheshaji namba moja
Wageni waalikwa na Mshereheshaji namba mbili
Wageni Waalikwa
Wageni Waalikwa
Wageni Waalikwa
Wanahabari wakiteta
Wageni waalikwa
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana akiongoza msafara kwa ajili ya Chakula cha Usiku.

No comments:

Powered by Blogger.