LIVE STREAM ADS

Header Ads

BAADHI YA WANACHAMA WA CCM KATA YA ILEMELA WAANDAMANA KUPINGA MATOKEO YA MGOMBEA UDIWANI.

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Ilemela Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, Wakiwa na mabango yao baada ya hii leo kuandamana hadi katika Ofisi za chama hicho Mkoa, wakishinikiza jina la mgombea wa Udiwani lililopitishwa katika kura za maoni katika Kata hiyo kurudishwa baada ya kukatwa katika Vikao vya Halmashauri Kuu Mkoa wa Mwanza kutokana na sababu kadhaa.
Majina ya Wagombea ngazi ya Udiwani Wilaya ya Ilemela yalitangazwa jumanne wiki hii.
Binagi Media Group
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Ilemela Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, hii leo wameandamana hadi katika Ofisi za chama hicho Mkoa, wakishinikiza jina la mgombea wa Udiwani lililopitishwa katika kura za maoni katika Kata hiyo kurudishwa baada ya kukatwa katika Vikao vya Halmashauri Kuu Mkoa wa Mwanza kutokana na sababu kadhaa.

Wakizungumza katika ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza, Wanachama hao walieleza kusikitishwa na maamuzi yaliyochukuliwa katika vikao hivyo vya Halmashauri Kuu baada ya kumpitisha aliekuwa mshindi wa pili katika Kura za maoni zilizofanyika hivi karibuni huku jina la aliekuwa mshindi wa kwanza katika kura hizo likiwekwa pembeni.

Walisema kuwa katika Uchaguzi wa kumpata mgombea wa nafasi ya Udiwani Kata ya Ilemela, Abeil Kaitira aliibuka na ushindi wa Kura 342 lakini katika vikao vya kupitisha majina ya wagombea, jina lake lilikatwa na nafasi yake kuchukuliwa na Wilbad Kilenzi aliekuwa mshindi wa pili katika kura za maoni kwa kupata kura 128.

“Eti wanatuambia kuwa jina la Kaitira limekatwa kwa kuwa hana makazi katika Kata anayogombea jambo ambalo si kweli kwani familia yake inakaa Mtaa wa Lumala. Pia wanasema eti hawezi kugombea udiwani katika Kata ya Ilemela kwa kuwa anafanya kazi Dar es salaam, sidhani kama Katiba ya CCM inamzuia mtu kugombea kwa sababu za kufanya kazi eneo tofauti na anapogombea”. Alisema Juma Bugingo ambae ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Butuja aliekuwa kiongozi wa maandamano hayo.

Huku kila mmoja akipaza sauti na kuimba wimbo wa “Tuna Imani na Kaitira”, Wanachama hao wamesema kuwa wako tayari kufanya maamuzi magumu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ikiwa jina la mgombea wanaemtaka ambae ni Abeil Kaitika halitarejeshwa.

Hata hivyo wanachama hao walishindwa kuonana na Uongozi wa CCM Mkoa, baada ya Msaidizi wake kuwaelezwa kuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu yuko Mjini Dodoma kwa ajili ya shughuli za kichama na waliweza kutawanyika baada ya mazungumzo ya ndani katika Ofisi za CCM Mkoa.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Ilemela Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, Wakiwa na mabango yao baada ya hii leo kuandamana hadi katika Ofisi za chama hicho Mkoa, wakishinikiza jina la mgombea wa Udiwani lililopitishwa katika kura za maoni katika Kata hiyo kurudishwa baada ya kukatwa katika Vikao vya Halmashauri Kuu Mkoa wa Mwanza kutokana na sababu kadhaa.
Majina ya Wagombea ngazi ya Udiwani Wilaya ya Ilemela yalitangazwa jumanne wiki hii.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Ilemela Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, Wakiwa na mabango yao baada ya hii leo kuandamana hadi katika Ofisi za chama hicho Mkoa, wakishinikiza jina la mgombea wa Udiwani lililopitishwa katika kura za maoni katika Kata hiyo kurudishwa baada ya kukatwa katika Vikao vya Halmashauri Kuu Mkoa wa Mwanza kutokana na sababu kadhaa.
Majina ya Wagombea ngazi ya Udiwani Wilaya ya Ilemela yalitangazwa jumanne wiki hii.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Ilemela Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, Wakiwa na mabango yao baada ya hii leo kuandamana hadi katika Ofisi za chama hicho Mkoa, wakishinikiza jina la mgombea wa Udiwani lililopitishwa katika kura za maoni katika Kata hiyo kurudishwa baada ya kukatwa katika Vikao vya Halmashauri Kuu Mkoa wa Mwanza kutokana na sababu kadhaa.
Majina ya Wagombea ngazi ya Udiwani Wilaya ya Ilemela yalitangazwa jumanne wiki hii.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Ilemela Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, Wakiwa na mabango yao baada ya hii leo kuandamana hadi katika Ofisi za chama hicho Mkoa, wakishinikiza jina la mgombea wa Udiwani lililopitishwa katika kura za maoni katika Kata hiyo kurudishwa baada ya kukatwa katika Vikao vya Halmashauri Kuu Mkoa wa Mwanza kutokana na sababu kadhaa.
Majina ya Wagombea ngazi ya Udiwani Wilaya ya Ilemela yalitangazwa jumanne wiki hii.
Hivyo Yani!!!!!
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Ilemela Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, Wakiwa na mabango yao baada ya hii leo kuandamana hadi katika Ofisi za chama hicho Mkoa, wakishinikiza jina la mgombea wa Udiwani lililopitishwa katika kura za maoni katika Kata hiyo kurudishwa baada ya kukatwa katika Vikao vya Halmashauri Kuu Mkoa wa Mwanza kutokana na sababu kadhaa.
Majina ya Wagombea ngazi ya Udiwani Wilaya ya Ilemela yalitangazwa jumanne wiki hii. Kwa mbaali Kikosi cha kuzuia ghasia kikiwacheki.
Msaidizi wa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Silaji Madebe (Kushoto) akitoa taarifa kwa wanachama hao ya kwamba hawataweza kuonana na Katibu kwa kuwa yuko Mjini Dodoma kwa ajili ya shughuli za kichama.

No comments:

Powered by Blogger.