KAIMU MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA NA MTATHIMINI WA JIJI HILO WAPANDISHWA KIZIMBANI.
"Wala Msiwe na Wasiwasi, nyie pigeni tu picha". Alikuwa akisema Mahinya (Wa kwanza) baada ya kutoka kusomewa mashtaka.
Na:Binagi Media Group
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Jeremiah Tito Mahinya pamoja na Mtathimini wa
Jijini hilo Ramadhan Seleman Kamese, wamepandishwa Kizimbani na kusomewa mashtaka ya tuhuma
zinazowakabili za kutumia vibaya madaraka kwa kuidhinisha kiasi cha
shilingi Milioni 161 kama vidia ya viwanja.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya
Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Mwema Mella, aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi Kanda ya Mwanza kuwa mwaka 2012 watuhumiwa hao walitumia vibaya
madaraka yao kwa kuidhinisha kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kulipa fidia za
viwanja katika eneo la Ilamba B, Nyamhongolo Jijini Mwanza bila idhini ya
Mtathimini Mkuu wa Serikali.
Baada ya Kusomewa mashtaka hayo,
watuhumiwa wote walikana tuhuma zinazowakabiri ambapo wameachiwa huru kwa kila
mmoja kudhaminiwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja ametakiwa kutoa Shilingi
Milioni 80 au mali isiyohamishika yenye thamani sawa na kiasi hicho cha fedha.
Kesi hiyo ambayo imekamilika upepelezi
wake kwa upande wa Mashtaka, iliahirishwa na Hakimu Mfawidhi Mkoa wa Mwanza Wilbert
Chuma hadi tarehe Saba Mwezi wa Tisa Mwaka huu itakapotajwa tena kwa mara ya
pili.
No comments: