LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANAHABARI ARON MIKOMANGWA AAPISHWA KUWA CHIFU WA WASUKUMA MKOANI MWANZA.

Chifu wa Wanang'wanza kutoka Kabila la Wasukuma, Koo ya Bahindi Mkoani Mwanza Aron Mikomangwa, Nyamironda III (Alievaa Kofia ya ngozi) Juzi Jumamosi akiwasili eneo la Airpot Ilemela Mkoani Mwanza kwa ajili ya kuapishwa rasmi ili kuitumikia nafasi hiyo na kuwa chifu wa 23 wa Wanang'wanza kutoka Koo ya Bahende kabila la Wasukuma.
Na:Binagi Media Group
Chifu wa Wanang'wanza kutoka Kabila la Wasukuma, Koo ya Bahindi Mkoani Mwanza Aron Mikomangwa, Nyamironda III Alizaliwa Mwaka 1960 katika Kijiji cha Nyashana, Kalebezo Wilayani Sengerema. 

Ni msomi wa Uandishi wa Habari, Mawasiliano na Ufundi Mitambo ya sauti (Sound Engenering) akiwa amepata mafunzo ndani na nje ya Tanzania.

Amefanya kazi na mashirika pamoja na taasisi mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha SAUT tawi la Mwanza, Fupi mitambo katika Studio ya Kanisa la AICT, Mwandaaji wa Vipindi mbalimbali vya radio vilivyokuwa vikirushwa na Radio Tanzania (Kwa sasa TBC Taifa, Radio Free Africa Chama cha Wanahabari Mkoa wa Mwanza na Mkurugenzi wa Studio ya Mass Media and Information na nyinginezo nyingi.

Mbali na shahada katika tasnia nyingine, ana Shahada mbili za Uandishi wa Habari na Sasa anasoma Shahada ya Uzamivu na hivyo anakuwa mmoja wa Machifu Wasomi. Mwaka 1990 alifunga ndoa na ana Mke na Watoto watatu.

Viongozi mbalimbali akiwemo mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Afisa Utamaduni Wilaya ya Ilemela na Mkuu wa Wilaya ya Iringa walioalikwa katika shughuli hiyo, walimpongeza Chifu Nyamironda III huku wakimhimiza kutumia nafasi hiyo kuwaweka karibu wale anaowaongoza katika kudumisha amani ya Taifa na kuendelea kuzienzi mila na desturi za Kitanzania.
Huu Mti ni Mahususi kabisa kwa ajili ya kuwaapishia Machifu. Unapatikana Airport Ilemela Mkoani Mwanza.
Picha ya pamoja
Hapa akielekea katika jiwe maalumu la kuapishia machifu ambalo linapatikana Ilemela
Shughuli ya Kumuapisha Chifu wa Wanang'wanza kutoka Kabila la Wasukuma, Koo ya Bahindi Mkoani Mwanza Aron Mikomangwa, Nyamironda III ikiendelea
Chifu wa Wanang'wanza kutoka Kabila la Wasukuma, Koo ya Bahindi Mkoani Mwanza Aron Mikomangwa, Nyamironda III Akiapishwa
Chifu wa Wanang'wanza kutoka Kabila la Wasukuma, Koo ya Bahindi Mkoani Mwanza Aron Mikomangwa, Nyamironda III Akiapishwa.
Chifu wa Wanang'wanza kutoka Kabila la Wasukuma, Koo ya Bahindi Mkoani Mwanza Aron Mikomangwa, Nyamironda III Akiapishwa
Shughuli imemalizika na sasa Chifu wa Wanang'wanza kutoka Kabila la Wasukuma, Koo ya Bahindi Mkoani Mwanza Aron Mikomangwa, Nyamironda III amekuwa Chifu kamili
Katikati ni Chifu wa Wanang'wanza kutoka Kabila la Wasukuma, Koo ya Bahindi Mkoani Mwanza Aron Mikomangwa, Nyamironda III 
Katikati ni Chifu wa Wanang'wanza kutoka Kabila la Wasukuma, Koo ya Bahindi Mkoani Mwanza Aron Mikomangwa, Nyamironda III
Ilikuwa ni furaha kubwa baada ya Chifu wa Wanang'wanza kutoka Kabila la Wasukuma, Koo ya Bahende Mkoani Mwanza Aron Mikomangwa, Nyamironda III kuapishwa juzi jumamosi na hivyo kuwa Chifu wa 23.
Na hapa ngoma zikiendelea nyumbani kwake Lumala, Kiseke, Ilemela Mkoani Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.