LIVE STREAM ADS

Header Ads

MIRADI ITAKAYOZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA LEO.

Na:Shaban Njia & Vesterjtz
Wananchi katika Halmshauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kujitokeza kwa Wingi katika kuupokea Mwenge wa Uhuru siku ya leo wakati ukifungua shughuli za Maendeleo katika Halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa Halmashuri ya Kahama Felix Kimaryo alisema hayo jana wakati akizungumza na Wanahabari na kuongeza kuwa Mwenge huo utapata fursa ya kukagua miradi 12 yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.3.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa kwa mwaka huu Halmashauri yake imejiandaa vyema katika miradi mbalimbali ya maendeleo hususani katika zoezi zima la ujenzi shule za Sekondari pamoja na maabara zake.

Kimaryo aliitaja baadhi ya miradi itakayokaguliwa na Mwenge huo kuwa ni pamoja na miradi ya kilimo cha Umwagiliaji katika Kijiji cha Lowa chalya, mradi wa jengo la Utawala katika Kijiji cha Kinaga na Miradi wa Maabara.

Miradi Mingine ni Ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami katika barabara ya Nyahanga, uhamasishaji wa Uchaguzi wa Madiwani, Wabunge na Urais pamoja na kuzindua vikundi vitatu vya hamasa katika Halmashauri hiyo.

Pia Mwenge huo utazindua Klabu ya kupinga utoaji wa na upokeaji wa Rushwa, Mradi wa Utunzaji wa Mazingira kwa kutumia Samadi (Biogas) pamoja na uzinduzi wa Mradi wa Bwawa la Samaki katika Shule ya Sekondari ya Quen of Familly iliyopo katika Kata ya Mwendakulima.

Hata hivyo aliendelea kuitaja miradi mingine kuwa ni uzinduzi wa wa Wodi ya akina mama katika Kata ya Kagongwa, Miradi ya Vijana na Wanawake wajasiriamali, Ushauri nasaha na upimaji wa Hiyari Virusi vya Ukimwi  pamoja na Mradi wa kupinga matumizi ya dawa za kulevya.

No comments:

Powered by Blogger.