LIVE STREAM ADS

Header Ads

MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MZEE SAMUEL LUANGISA YAFANYIKA NEW YORK NCHINI MAREKANI.

Mchungaji Butiku akiongoza misa ya shukurani na arobaini ya marehemu Mzee Samuel Luangisa iliyofanyika siku ya Jumamosi Aug 8, 2015 Mount Vernon, New York na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki kutoka kila pembe ya Marekani. 
Mzee Luangisa enzi za uhai wake alikuwa ni miongoni mwa waasisi wa Taifa na katika vipindi tofauti alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi(Kagera)Mbunge na Meya wa Manispaa ya Bukoba pamoja na nyadhifa nyingine.
Na:Kwanza Productin
Mrs Luangisa, mke wa marehemu akifuatilia misa.

Wanafamilia wakifuatilia misa.

Wajukuu wa marehemu wakifanya onesho la kumuenzi babu yao.

Mtoto wa marehemu Mao Luangisa akitoa salamu za shukurani.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York Hajji Khamis akiongea machache huku akisisitiza upendo na mshikmano kwenye Jumuiya za Watanzania hususani zile zilizopo nje ya Tanzania kwani kwa kufanya hivyo Jumuiya zitakua imara.

Mchungaji Butiku akiongoza misa.

Wakati wa maakuli.
Kwa picha zaidi bofya HAPA

No comments:

Powered by Blogger.