LIVE STREAM ADS

Header Ads

ILIVYOKUWA BALAA KATIKA MAONYESHO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI NANENANE KANDA YA ZIWA.

Huu ni Umati wa Wananchi uliojitokeza Jana Agosti 08, 2015 Katika Maonyesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yaliyofanyika Kwa Kanda ya Ziwa katika Viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza.
Mgeni Rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Stanslaus Mulongo ambapo katika Hotuba yake ya kufunga Maonyesho hayo alisisitiza kuwa Maonyesho hayo yanapaswa kuboreshwa zaidi ikiwa ni pamoja na Uwanja wa Nyamhongolo kuboreshwa zaidi.
Na:George GB Pazzo
Umati wa Wananzengo ukifuatilia burudani kutoka kwa mmoja wa wasanii wa nyimbo za Asili kutoka Igoma Igoma Jijini Mwanza.
Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel nayo iliwapagawisha wateja wake kwa huduma mbalimbali ikiwemo ofa za simu na line zake na zawadi za tshirt bila kusahau burudani ile kinoma noma
Airtel ilikuwa hatareeeeee
Umati wa Wananchi ukifuatilia burudani kutoka katika Banda la Airtel katika Maonyesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza.
Kampuni ya Ving'amuzi ya StarTimes nayo ilikuwa ikitoa huduma zake kwa wananchi na wateja wake.
Kampuni ya Ving'amuzi ya Continental nayo ilikuwepo
Kapuni ya Uuzaji na Wakopeshaji wa Mitambo ya kuzalisha Umeme wa Jua (Solar) ya Mobisol nayo ilikuwepo na hapa wananchi walikuwa wakipata huduma mbalimbali kutoka Mobisol.
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT pia kilikuwepo
Mtambo wa Kurushia Matangazo ya Moja kwa Moja katika Runinga ulikwepo katika banda la Chuo Kikuu cha SAUT
GB Pazzo (Mwenye Kofia) akitest Mtambo wa Kurushia matangazo ya moja kwa moja katika Banda ya Chuo Kikuu cha SAUT Mwanza.
Kampuni ya Ving'amuzi ya StarTimes nayo ilikuwa ikitoa huduma zake kwa wananchi na wateja wake.
Wananzengo katika Viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza wakiwa katika pirikapirika za hapa na pale
Kampuni ya Nyanza Bottling ya Jijini Mwanza inayozalisha Vinywaji jamii ya Cocacola pia ilikuwepo kwa ajili ya kutoa huduma ya vinywaji na burudani kwa wananchi.
Timu ya Cocacola
Kampuni ya M-Power inayozalisha Umeme kwa kutumia nishati ya jua pia ilikuwepo na hapa wananchi wakihudumiwa.
Viwanja vya Nyamhongolo vilifurika watu.
Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo pia ilikuwepo kwa ajili ya kutoa huduma na burudani kwa wateja wake na wananchi kwa ujumla.
Mnyama aina ya Nyati
Hivyo ndivyo ilivyokuwa jana 08.08.2015 katika Maonyesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yaliyofanyika jana katika Viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza yakishirikisha Mikoa yote ya Kanda ya Ziwa.
Soma HAPA Habari Zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.