LIVE STREAM ADS

Header Ads

MJUMBE WA MKUTANO MKUU TAIFA NDANI YA CHADEMA APIGWA KATIKA KURA ZA MAONI NA MUUZA MBOGA MKOANI SHINYANGA.

Na:Shaban Njia
Mjumbe wa Mkutano Mkuu katika Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Sebastiani Mashinji(Komaa) ameburuzwa katika kura za maoni za kumpata mgombea Udiwani Kata ya Nyihogo.

Komaa alipata kura 10 kati ya kura 43 zilizopigwa na wajumbe wote ambapo Amosi Sipemba maarufu kama muuza mchicha aliibuka kidedea kwa ushindi wa kura 30.

Kura zilizopigwa ni 43 na hakuna kura iliyoharibika ambapo Amosi Sipemba alipata kura 30,Sebastiani Mashinji kura 10, Michael Ngaja kura 2 huku Hashimu Baraka akipata kura moja". Alisema Michael Kigenda ambae alikuwa msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo.

Akizungumza kwa niamba ya watiania walioshindwa katika kinyanganyiro hicho, Michael Ngaja alisema kuwa walioshindwa katika mchakato wa kumpata mgombea udiwani Kata ya Nyihogo watashirikiana na mshindi wa kinyang'anyiro hicho lengo likiwa ni kuwezesha chama kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa mwaka huu.

“Sisi tumekubali kushindwa katika kinyanganyiro cha kumtafuta mgombea mbae anawezo kuiongoza kata ya nyihogo ambapo wajumbe wameona kuwa anaeweza kuwasimamia na kuwatetea ni amosi sipemba hivyo basi hatuna budi kushirikiana nae kwa ukaribu kwani Chadema ni wamoja chini ya Kauli Mbio yetu ya Maendeleo kwanza na sio Marumbano na Chuki”. Alisema Ngaja.

Akitangaza matokeo ya viti maalum katika Kata hiyo pia Kigenda alimtaja Hamisa Siraji kuwa mshindi kati ya wagombea watano waliokuwa wakiwania kiti hicho ambapo alipata kura Sita na kufuatiwa na wagombea wengine ambao walikuwa ni Frida Rujuba aliepata kura tano, Anna Kabenywela aliepata Kura Tatu pamoja na Kulwa Mgaya aliepata kura mbili.

No comments:

Powered by Blogger.