LIVE STREAM ADS

Header Ads

HUU NDIO USHAURI MWINGINE ULIOTOLEWA KWA VIJANA HAPA NCHINI.

Wasanii wa kikundi cha Eagle Power cha Jijini Mwanza wakiwa wamevalia mavazi ya asili katika picha ya pamoja.
Judith Ferdinand  na Neema Emmanuel
Vijana nchini wamehimizwa kujiunga na vikundi mbalimbali vya sanaa, kwa lengo la kuendeleza vipaji vyao pamoja na kujipatia ajira kupitia vikundi hivyo.

Rai hiyo ilitolewa jana Jijini Mwanza na Mwenyekiti wa Kikundi cha Sanaa cha Eagle Power Abdalah Kutilingombe wakati akizungumza na waandishi.

Kutilingombe alisema kuwa hatua hiyo itawasaidia vijana kujikwamua kiuchumi na kuacha kulalamikia serikali kutokana na ukosefu wa ajira jambo linalowashawishi vijana wengi kujiingiza katika uharifu.

Pia alisema kuwa kikundi hicho kinawakaribisha vijana kujiunga nacho ambapo alibainisha kuwa tayari kimerekodi filamu nyingi japo iliyokamilika kurekodi  ni moja ambayo ilipelekwa kwa wasambazaji na kukataliwa kutokana na kutokuwa na  bora kwa vile wanatumia waongozaji wa mtaani wasiokuwa na vifaa vya kisasa pamoja na taaluma jambo ambalo linatokana na msukumo wa kikundi kutokuwa na  fedha.  

Naamini tukipata wadhamini tutaleta mabadiliko katika sanaa na hatimae kuteka Soko lake ndani na nje ya nchi kwani kundi letu lina watunzi na wasanii wazuri". Alisema Kutilingombe.

Naye mmoja wa  wanakikundi hicho Rukia Said  aliwaomba vijana kuipenda, kuiheshimu na kushiriki katika Sanaa ili kujikwamua kiuchumi.
Picha wasanii wa kikundi cha Eagle Power cha Jijini Mwanza wakiwa wamevalia mavazi ya asili katika picha ya pamoja.
Picha wasanii wa kikundi cha Eagle Power cha Jijini Mwanza wakiwa wamevalia mavazi ya asili katika picha ya pamoja.
Picha zote na Judith Ferdinand

No comments:

Powered by Blogger.